Siku 100 za Trump Madarakani: ashambulia vikali wanahabari aelezea mafanikio yake!


Rais wa Marekani Donald Trump ameadhimisha siku mia moja uongozini kwa kutoa hotuba ya kushambulia wanahabari na kutetea mafanikio yake.
Bwana Trump amewaaambia wafuasi wake huko Pennsylvania kwamba ameridhika kuwa pamoja nao badala ya kuhudhuria dhifa ya chakula cha jioni na wanahabari ama 'Correspondents diner' iliyokuwa ikifanyika katika ikulu ya White House wakati huo.
Hafla hiyo ni miongoni mwa hafla maarufu sana mjini Washington.
Akihutubia umati mkubwa katika jimbo la Pennsylvania, Rais Trump amelinganisha na kutofautisha, kile ametaja 'siku mia moja za wanahabari kushindwa na kazi yao', na mafanikio yake ambapo amesema amekuwa akitimiza 'ahadi zake kila siku', hususan kurejesha kazi za viwanda na kumaliza mzozo katika sekta ya makaa ya mawe.
Pennsylvania ni jimbo linalotegemea uchumi wa uchimbaji madini, na lilikuwa muhimu sana katika uchaguzi wa mwaka jana.
Awali maelfu ya watu waliandamana nchini Marekani dhidi ya utawala wa rais Trump na msimamo wake kuhusu mazingira - bbc swahili 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search