GOOGLE kuvunja rekodi ya Kulipa 'faini' ikiilipa EU dola 2.7 Bilioni.. #share

Google imepigwa faini ya ya dola bilioni 2.7 na tume ya ulaya baada ya tume hiyo kuamua kuwa Google ilikuwa imekiuka mamlaka yake ya kuweka matangazo yake binafasi kuwa ya kwanza.
Faini hiyo ndiyo kubwa zaidi iliyotolewa na tume ya ulaya hadi leo, kwa kampuni ambayo imelaumiwa kwa kukiuka sheria za biashara.

Amri hiyo pia inataka Google kundoa vizingiti vinavyozuia ushindani ndani ya kipindi cha siku 90 la sivyo ichukuliwe hatua zaidi, Hata hivyo kampuni hiyo ya Marekani inasema huenda ikakata rufaa.
Tume ya Ulaya ilisema inaiachia Google jukumu la kuamua ni mabadiliko yapi itafanyia mifumo yake ya mauzo.
"Kile ambacho Google imekifanya na haramu chini ya sheria za EU," alisema Margrethe Vestager, kamishina wa ushindanii wa kibiashara wa tume ya EU.
Tume ya Ulaya imekuwa ikichunguza mifumo ya biashara ya Google tangu mwaka 2010, Uchunguzi huo ulianza kufuatia malalamiko kutoka makampuni kama Microsoft miongoni mwa mengine.
Hata hivyo Microsoft hajatoa tamko lolote kufuatia uamuzi huo baada ya mahasimu hao kufikia makubaliano ya kujaribu kuzuia kesi mahakamani siku za usoni.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search