CCM wampitisha Mtulia, Mollel kugombea ubunge Kinondoni, Siha...soma habari kamili na matukio360..#share

Na mwandishi wetu, Dar es salaam

KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kwa mamlaka iliyokasimiwa kwake na kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) imewateua Godwin Mollel kugombea ubunge jimbo la Siha, Kilimanjaro na Maulid Mtulia kugombea jimbo la Kinondoni, Dar es Salaam.

Maulid Mtulia


Mtulia aliyekuwa mbunge wa Kinondoni kwa tiketi ya CUF na Mollel aliyekuwa mbunge wa Siha kwa tiketi ya Chadema, hivi karibuni wote walitangaza kujiuzulu nyazifa zao na kuhamia CCM kwa madai kuwa ni kuunga mkono juhudi  za Rais John Magufuli katika kupigania rasalimali za nchi. 

Uchaguzi wa marudio wa majimbo hayo utafanyika Februari 17, 2018



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search