Jose Mourinho kuongeza mkataba Man U ....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa

KLABU  ya Manchester United inakaribia kufikia makubaliano na kocha wake, Jose Mourinho wa kuongeza mkataba mpya.


Jose Mourinho
Mazungumzo kati ya pande hizo mbili yanaendelea vyema na ni suala la muda tu kabla ya Mourinho hajaongeza mkataba mpya klabuni hapo na mkataba wake wa sasa unafikia ukingoni mwaka 2019.
Taarifa za ndani ya klabu zinaeleza kuwa kama kocha huyo atasaini mkataba mpya utamuweka klabuni hapo hadi mwaka 2021.
Licha ya kulaumiwa na wachambuzi wengi wa soka pamoja na washabiki wa klabu ya Man kuwa timu hiyo inacheza mchezo wa kujilinda bado viongozi wa United wanaona kuwa Mourinho anaweza ibeba timu hiyo katika kuipa mataji makubwa barani ulaya.
Mourinho alijiunga na United mwaka 2016 kuchukua mikoba ya Luis Van Gaal, ameisadia Man United kutwaa ubingwa mwa kombe la Europa na Lile la EfL Carabao.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search