Mahakama yaombwa imuonye wakili wa Masogange ...soma habari kamili na matukio 360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
UPANDE wa mashtaka katika kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili, Agnes Gerald  ‘Masogange’ umeitaka mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kuuonya upande wa utetezi kuchelewesha kesi hiyo.

Agnes Gerald 'Masogange' aliyevaa miwani.

Ombi hilo limetolewa na upande wa mashtaka kutokana na upande wa utetezi kushindwa kutoa ushahidi wao kwa mara ya tatu mfululizo.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa utetezi, Nehemia Nkoko kudai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri kuwa Wakili mwenzake anayemtetea Mshtakiwa Msogange, Reuben Simwanza, ndiye aliyeandaa mashahidi lakini ameshindwa kufika kwa kuwa anaumwa.

Nkoko amongeza, atahakikisha anaandaa mashahidi ili ikitokea wakili mmoja wao hayupo, mwengine aendelee na kesi.

Wakili wa Serikali,  Constantine Kakula alidai kuwa hawana pingamizi na sababu zilizotolewa na upande wa utetezi lakini wanaomba mahakama itambue kuwa ni mara ya tatu kesi kwa upande wa utetezi inaahirishwa.

"Mawakili wapo wengi lakini wanashindwa kuendelea kutoa ushahidi wao wa upande wa utetezi basi kama hawawezi, waache mshitakiwa aendelee na kesi mwenyewe," alidai Kakula.

Pia aliiomba mahakama kutoa ahirisho la mwisho kwa sababu kesi ni ya muda mrefu. Kutokana na hali hiyo, Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 26, mwaka huu  kwa ajili ya kusikilizwa.

Masogange ataanza kujitetea baada ya mahakama kumkuta na kesi ya kujibu baada ya kusikiliza mashahidi watatu wa upande wa mashitaka.

Masogange anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14, mwaka jana katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine).


Pia anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14, 2017 alitumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search