Serikali yaagiza kupitiwa upya mkataba Polisi na Ashoki Leyland...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
SERIKALI imeagiza kupitiwa upya mkataba wa ununuzi wa magari ya jeshi la
polisi nchini na Kampuni ya kutengeneza magari ya Ashoki Leyland ya nchini India
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Hamad Masaun akifafanuliwa jambo na Kaimu Meneja wa Bandari, Fredi Liundi jijini Dar es Salaam.
Hamad Masaun akifafanuliwa jambo na Kaimu Meneja wa Bandari, Fredi Liundi jijini Dar es Salaam.
Pia imeagiza uundwajia tume ya wataalam kuchunguza ubora wa magari
53 maarufu ya Magufuli yaliyotolewa bandarini na kupelekwa chuo cha polisi Kurasini baada
ya kubainika magari matano kuwa mabovu.
Maagizo hayo yametolewa leo jijini Dar es Salaam na Naibu
waziri wa wizara hiyo, Hamad Masaun alipofanya ziara ya kuona utekelezaji wa
maagizo ya Rais John Magufuli ya kuyaondoa magari hayo bandarini kwenda mahali
husika kwa ajili ya matumizi iliyokusudiwa.
“Magari mengi niliyoyaona hapa ni maroli, lakini tunahitaji
magari madogo pia, nitoe maalekezo kwa katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani
ya nchi, kuundwa kamati ya wataalamu kuangalia mkataba wa utaratibu wa jinsi ya
uingizaji magari haya,” amesema Masaun.
Amesema kamati hiyo itapata nafasi ya kukaa pamoja na
wasambazaji hao ili kuupitia makataba kwa ajili ya maslahi ya pande zote lakini
pia kuona kama unakidhi mahitaji ya sasa.
Akizungumzia hatua ya kuagiza kuundwa kwa tume ya wataalamu
wa kuchunguza ubora wa magari hayo 53, amesema agizo hilo limekuja kutokana na
mashaka juu ya magari hayo baada ya kupata maelezo kutoka kwa kampuni ya Ashoki
Leyland juu ya ubovu wa magari hayo
matano kutokana na uchunguzi wao.
Katika hatua nyingine ametaka magari mengine 119 ambayo bado
yapo bandarini yaliyoingia baada ya agizo la rais Magufuli, kufanyiwa utaratibu
wa haraka wa kuyaondoa ili yakatumike.
Mwishoni mwa mwaka jana rais Magufuli alifanya ukaguzi wa
ghafla Bandari ya Dar es Salaam na kukuta magari 53 aina ya Suzuki ambayo ni
maalumu kwa kubebea wagonjwa na maroli zaidi ya 50 ya jeshi la polisi
yaliyoagizwa tangu mwaka 2015 lakini yalikuwa bado hayajatolewa bandarini.




No comments:
Post a Comment