Staa Jacqueline Wolper’ ‘Vyamshuka’ baada ya madai ya kunuka mwili’.. asema ‘Mbona Mabwana Wananipapatikia..!’


Staa wa filamu ‘grade one,Jacqueline Wolper’ ametokwa povu si la nchi hii baada ya kubanwa kuhusiana na madai ya kunuka mwili na kusema hajawahi kunuka maishani mwake na kwamba ingekuwa hivyo asingepapatikiwa na wanaume. Hivi karibuni gazeti la mambo ya udaku la global Ze Ijumaa, lilimfungia kazi msanii huyo nyumbani kwake na katika moja ya maswali aliyobanwa lilikuwa juu ya ishu iliyosambaa kuwa eti anatoa harufu mbaya sehemu za mwili wake.

Katika kuonesha kumaindi ile mbaya kuhusu madaia hayo, mrembo huyo ambaye kiukweli yuko bomba kwa muonekano alifunguka: “Aliyekuambia nanuka nani? Mimi sinuki wala sijawahi kunuka maishani mwangu, kuthibitisha hilo kwanza nisingekuwa napapatikiwa na wanaume kila kukicha sambamba na kuhongwa vitu kibao huku wengine nikiwaacha wakinililia.


Hao wanaosema na kusambaza hayo ni njia tu ya kujipatia followers kwenye mitandao yao kupitia nyota yangu”…  Wolper hakuishia hapo aliendelea kumwaga povu kuwa, tangu afungue duka lake nguo ambalo amewekeza zaidi ya shilingi milioni 60, watu wengi wamekuwa wakichukizwa na maendeleo hayo. “Wana chuki tu na mimi, tangu nimefungua duka wananichokonoa, wanalishadadia hili jambo kisa tu nimepata mafanikio ya kufungua duka,” alipigilia msumari.

credit: QON na global 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search