MORNING News: Ulinzi umeimarishwa Lowasa akiwasili kwa DCI mda huu.. Kairuki awaonya watumishi kuvujisha siri za Serikali... #share Waliomchojoa nguo bidada wahukumiwa kinyongo,..
![]() |
cover foto - Waziri Mkuu Msataafu Bw. Edward Ngoyai Lowasa |
Serikali imewaonya Watumishi wa Umma ambao wanapokea na kuzitoa siri za Serikali kisha kuzisambaza katika mitandao ya kijamii ikisema hilo ni kosa kubwa na adhabu yake ni zaidi ya miaka 20 jela kwa mujibu wa Sheria ya Usalama wa Taifa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki amewaonya Watumishi wa Umma wanaopokea taarifa za serikali kinyume na sheria wazifute pamoja na kwamba kutaka kuonekana wa kwanza kusambaza taarifa.
”Sisemi kwa vitisho lakini Serikali inawafatilia Maofisa na Watumishi waliovujisha taarifa za watu wenye vyeti vyenye utata kwani hao ndio wenye password na ndio walioingia kwenye mfumo uliokuwa na tangazo, mtashuhudia tu kitakachowapata muda si mrefu.”
Kwa upande mwingine, Waziri Kairuki amewataka Watumishi kufanya kazi kwa kufuata maadili mema ili kuwa mfano wa kuigwa kwa wengine, pamoja na kuwa wabunifu na waadilifu na kutofanya kazi kwa mazoea akiwataka pia kuwahudumia Watanzania kwa staha bila kujali vyama, dini na hali zao za kipato.
========================
Mahakama moja ya Nairobi, siku ya Jumatano iliwahukumu wanaume watatu kunyongwa, baada ya kupatikana na hatia ya kumvua nguo mwanamke mmoja, kumdhalilisha na kujaribu kumbaka...
Kisa hicho kiltokea wakati wa wimbi la uvamizi wa wanawake miaka mitatu iliyopita, ambapo makundi ya watu yalikuwa yakidai kwamba wanawake walikuwa wanavaa mavazi yasiyokubalika.
Wabanawake wa Kenya waandamana kupinga udhalilishwaji unaotekelezwa na baadhi ya makundi ya watu yanayopinga jinsi walivyovalia nguo zao.
Watu hao watatu walipatikana nahatia ya wizi wa kutumia nguvu, ambao hukumu yake ni kifo.
Hata haivyo, sheria ya hukumu ya kunyongwa nchini Kenya haijatekelezwa tangu mwaka wa 1987, na hukumu kama hizo zimebadilishwa na kuwa vifungo vya maisha.
Baadhi ya visa vya uvamizi huo, ambavyo vilikithiri mnamo mwaka wa 2014 vilirekodiwa kwanye simu za mkono, na kupelekea maandamano, huku waliokuwa wakipinga vitendo hivyo - wengi wao wakiwa wanawake - wakianzisha hashtag iliyoitwa #MyDressMyChoice kwenye mitrandao ya kijamii.
Muathiriwa huyo aliiambia mahakama kwamba wanaume hao watatu walikuwa kati ya kundi la wanaume saba waliotaka kumbaka ndani ya basi, lakini wakakaachana naye alipowaambia kwamba alikuwa na virusi vya ukimwi. ================================================
DAR: Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa awasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kwaajili ya kuendelea na mahojiano na Ofisi ya DCI#JFLeo pic.twitter.com/SR8Bg5ZxWY— Jamii Forums (@JamiiForums) July 20, 2017
Ulinzi mkali umeimairishwa, Waziri Mkuu wa zamani E. Lowassa akiwa ndani Makao Makuu ya Polisi, waandishi wa Habari watakiwa kusogea mbali pic.twitter.com/yd22cikDFy— Mwananchi Newspapers (@MwananchiNews) July 20, 2017
Taarifa ya Uteuzi wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji @kitilam pic.twitter.com/4ZFwi2Xy3i— Sheila simba (@Mercy_Simba) July 19, 2017
==============================================
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amewasili leo, Julai 20 saa mbili asubuhi makao makuu ya Jeshi la Polisi kwenye ofisi za Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz.
Lowassa ameambatana na mkewe, Regina na mwanasheria wake, Peter Kibatala.
Hii ni mara ya nne kwa Lowassa kuripoti hapo akituhumiwa kutoa kauli za kichochezi wakati wa futari iliyoandaliwa Juni 23, na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.
Katika futari hiyo, Lowassa anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi kuhusu masheikh wa Taasisi ya Uamsho wanaoshikiliwa gerezani akidai utaratibu wa kisheria ufanyike ili waachiwe huru.
Polisi wameimarisha ulinzi eneo hilo, huku Lowassa akiwa ndani tayari kwa kuhojiwa.
Lowassa aripoti kwa DCI https://t.co/6tZekEdcp2 via @MwananchiNews— Mwananchi Newspapers (@MwananchiNews) July 20, 2017
Use #bbcfootball— BBC Sport (@BBCSport) July 20, 2017
Lacazette > Arsenal £46.5m
Lukaku > Man Utd £75m
Morata > Chelsea £60m
Who's the best value & why? https://t.co/EEAjcZErSq pic.twitter.com/g4uO4dV9HU
#Habari:Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa awasili Polisi Makao Makuu Dar kwa mahojiano, ulinzi waimarishwa,waandishi watakiwa kukaa mbali pic.twitter.com/c6GZLVyr0u— Radio One Stereo (@RadioOneStereo) July 20, 2017
LOWASSA RELEASED:Former Premier Edward Lowassa leaves Police Headquarter in Dar, as investigation continues, his lawyer Peter Kibatala says pic.twitter.com/FDYWfbBrfR— The Citizen Tanzania (@TheCitizenTZ) July 20, 2017
Utata waibuka dhamana ya Dk Mashinji, wenzake nane https://t.co/yymOWIZQyb via @MwananchiNews— Mwananchi Newspapers (@MwananchiNews) July 20, 2017
No comments:
Post a Comment