Breaking: Tundu Lissu amuibua IGP Sirro na mkakati mzito kuwatia mbaroni wahalifu.. na wateule waliotajwa 'makinikia' hakuna kulala.. #share

SIKU moja baada ya Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kupigwa risasi akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma, Mkuu wa Jeshi la Polish nchini IGP Simon Sirro ameunda timu ya upelelezi kutoka Makoa Makuu ya jeshi hilo kuongeza nguvu ili kuwakamata wahusika.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na IGP Sirro akizumza na waandishi wa Habari, amesema timu hiyo imefika mkoani Dodoma tangu jana na kubainisha kuwa wamejipaka kuhakikisha waliofanya kitendo hicho wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
"Kufuatia tukio hilo, nimeunda timu ya upelelezi Kutoka Makao Makuu ya Polisi ambayo ilishafika mkoani Dodoma Jana kuongeza nguvu ili kuhakikisha kuwawatuhumiwa waliofanyakitendo hicho wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria," amesema IGP Sirro.
Aidha amesema kufuatia tukio hilo, wananchi walianza kusambaza taarifa mbalambali kwenye mitandao ya kijamii ambazo zinaibua hofu kwa Jamii na zinaweza pia kuharibu upelelezi pamoja na kujenga chuki na mtafaruku kwa Jamii.
IGP Sirro ametoa rai kwa wananchi kuacha kusambaza ujumbe, picha, video na taarifa zisizo na ukweli kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na Matukio kama hayo kwani ni kosa la kisheria. Amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo katika katika kutoa taarifa zitakazo saidia kukamata watuhumiwa.
Kwa upande mwingine IGP Sirro amesema jeshi hilo limeanza kuchukua hatua kwa kuwakamata watuhumiwa waliotajwa katika ripoti ya Madini ya Almasi na Tanzanite iliyokabidhiwa Jana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwaRais John John Magufuli.
"Mheshimiwa Raid alitoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua kwa wahusika waliotajwa Kwenye ripoti hiyo," amesema Sirro.
Aidha amewataka wate waliotajwa katika ripoti hiyo kufika wenyewe kwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kwa ajili ya mahojiano na wasisubiri kutafutwa.
Amesema Jeshi hilo kwa kushirikiana na vyombo vingine tayari limeunda kikosi kazi cha kushughulikia ripoti hiyo huku akibainisha kuwa ambao wamekwisha kamatwa wanaendelea kohojiwa kwa lengo la kukusanya ushahidi na hatimaye wafikishwe mahakamani.
Na Abraham Ntambara
Mwisho

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search