UPDATES: Jua hapa safari nzima ya Tundu Lissu kuelekea Nairobi kwa matibabu ilivyokuwa...#share
Habari, Mh Tundu Lisu aliwasili usiku majira ya saa Saba hapa
Nairobi Jomo Kenyatta International Airport na alipokelewa na team ya Madaktari
wa Nairobi hospital pale airport na matibabu yalianza Mara moja kuanzia ndani
ya Ambulance hadi hospital.
Aidha alipofika Nairobi hospital alifanyiwa vipimo vyote na
baadae saa nne asubuhi aliingizwa theatre. Tangu Jana alipofika alifanyiwa
stabilization ili aweze kukabiliana na surgery na zoezi hilo lilifanikiwa
vizuri na madaktari wametueleza kuwa hakuna hali yoyote ya hatari na
matibabu yake yanaendelea kwa mafanikio.
Hadi sasa majira ya saa 9 alasiri bado hajatoka theatre na
madaktari wametueleza kuwa wanaendelea vizuri. Nitawajuza atakapo toka theatre.
Chakushangaza hadi sasa tangu tuwasili hatujapata ushirikiano
wowote wa ubalozi wa Tanzania hapa Nairobi, Si kwa balozi au maafisa wowote
wale wa ubalozi. Mh Freeman Mbowe amezungumza na vyombo mbali mbali vya habari
pia taarifa yake itatoka punde.
Hemed Ali
Mkuu wa Idara ya Uenezi CHADEMA.
Nairobi hospital.




No comments:
Post a Comment