Kesi ya Madawa ya Kulevya ya Madam Wema: Inspekta Wille afunguka.. " chumbani kwa mahausegel tulikuta kiberiti chenye msokoto wa bange ambao umeshavutwa".. #share
Kesi ya kukutwa na dawa za kulevya, inayomkabili miss Tanzania wa mwaka 2006, Wema Sepetu, imeendelea leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa upande wa mashtaka kuendelea kusikiliza ushahidi.
Mbali na Wema, washtakiwa wengine katika kesi hiyo Angelina Msigwa na Matrida Seleman Abbas, wote wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.
Shahidi wa pili katika kesi hiyo, Inspekta Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Wille (43) kutoka ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalum ya Dar es Salaam amedai mahakamani hapo kuwa alifanikiwa kufanya upekuzi katika nyumba ya Wema na kukuta misokoto ya bangi chumbani kwake na dirishani.
Akiongozwa na wakili wa Serikali, Costanine Kakula mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, shahidi huyo alidai Februari 4,2017 anaikumbuka kwa sababu aliitwa na Mkuu wake wa kazi na kupewa kazi ya kufanya upekuzi nyumbani kwa Wema na aliongozana na WP Mary, Koplo Robert, PC Hassan na dereva kuelekea Unonio anapoishi Wema ili wakaufanye upekuzi huo.
Inspekta Wille alidai kuwa walipofika nyumbani kwa Wema huko Ununio waligonga mlango na kwamba waliwakuta wasichana wawili ambao ni wafanyakazi wa Wema na wakaomba waitiwe mjumbe wa nyumba kumi Steven Noho wakaitiwa.
Wille alidai kuwa walimueleza kuwa wamekwenda nyumbani kwa Wema kwa nia ya kufanya upekuzi nyumbani kwa Wema na wanatafuta dawa za kulevya na kitu chochote ambacho wangekitilia shaka.
Akiendelea kutoa ushahidi kwenye kesi hiyo, Inspekta Wille alidai kuwa upekuzi huo uliendelea katika chumba cha wasichana wa kazi wa Wema, walifanikiwa kukuta kiberiti ambacho ndani yake kulikuwa na msokoto ambao unaonekana umeishavutwa.
Katika kesi ya msingi, inadiawa kuwa Februari 4,2017 katika Makazi ya Wema huko Kunduchi Ununio washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.
Kwa upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa Februani Mosi, 2017 katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya Bangi.
Wema ni miongoni mwa watu waliotajwa na Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda wakituhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya.
Inadaiwa kuwa Februari 3, 2017, Wema alijipeleka mwenyewe katika Kituo cha Polisi Kati ambapo alikamatwa.

No comments:
Post a Comment