Yaliyojiri Kisutu Leo: Wakili Mutalemwa amuweka pabaya Halima Mdee kesi ya kumtusi Rais... Hakimu Nongwa apeleka October 11.. #share
Upande wa mashtaka katika kesi ya kumtolea lugha ya matusi Rais John Magufuli inayomkabili, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee umeieleza mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu kuwa, upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.
Wakili wa serikali mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa, leo kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.
Kishenyi amedai kuwa anaiomba mahakama hiyo, ipange tarehe kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali (PH).
Baada ya kusema hayo, wakili wa Mdee, Peter Kibatala alidai kuwa wanaondoa mapingamizi yao ya kwamba mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.
Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Nongwa aliahirisha kesi hiyo hadi October 11/2017 kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali.

No comments:
Post a Comment