Waziri Jafo aagiza halmashauri kuwa na duka la dawa....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Kisarawe

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo amezitaka Halmashauri kuanzisha maduka ya dawa katika wilaya zao ili kuondokana na tatizo la ukosefu wa dawa kwenye maeneo hayo.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akikagua madawa yaliyohifadhiwa katika stoo ya duka la kisasa la dawa.

Waziri Jafo ameitoa kauli hiyo leo alipokuwa akifungua duka la dawa la kisasa lililofunguliwa katika Hospitali ya wilaya ya Kisarawe ambapo duka linatarajiwa kuondoa tatizo la ukosefu wa dawa katika hospitali ya wilaya, vituo vya afya, na zahanati wilayani Kisarawe.

Akifungua duka hilo, Jafo amesema endapo dawa zitakosekana katika duka la hospitali au katika vituo vingine vya kutolea huduma ya afya wilayani basi watanunua dawa katika duka hilo.

Aidha amezitaka Halmashauri zingine kuiga mfano wa Halmashauriza Kisarawe, Muheza, Jiji la Tanga na zingine ambazo tayari zimejipanga vyema kuwahudumia vyema wananchi wao katika suala la Afya.

Waziri Jafo ameipongeza Bohari ya Dawa(MSD) kwa msaada mkubwa wanaoutoa katika kufanikisha uanzishaji wa maduka hayo ya dawa.

Duka hilo limeanzishwa kwa gharama ya sh. milioni 89 ambapo kiasi cha Sh.Milioni 10 alizitoa Jafo ambaye pia ni Mbunge wa Kisarawe na Sh.Milioni 79 zilitolewa na Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search