Shein afanya mabadiliko baraza la mawaziri Zanzibar....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwajuma Juma, Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri kwa kuanzisha Wizara mpya itakayoshughulikia masuala ya Vijana,Utamaduni,Sanaa na Michezo ambapo Balozi Ali Karume ameteuliwa kuongoza Wizara hiyo.
Rais Dk Ali Mohamed Shein
Katika mabadiliko hayo Hamad Rashid anakuwa Waziri wa Afya kutoka katika Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi ambapo naibu wake anaendelea kuwa Harusi Said Suleiman.
Aidha katika mabadiliko hayo aliyekuwa Waziri wa Habari Utalii na Michezo Rashid Ali Juma sasa anakuwa Waziri wa Kilimo Maliasili na Mifugo na Mahomud Thabit Kombo ambaye alikuwa Waziri wa Afya sasa anakuwa Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya kale.
Dkt Sira Ubwa Mamboya ambaye alikuwa Waziri asiye na Wizara maalumu sasa ameteuliwa kuongoza Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji,na kuchukuwa nafasi ya balozi Ali Karume ambaye ameteuliwa kuongoza Wizara mpya ya Vijana,Utamaduni na Sanaa na Michezo.
Katika mabadiliko hayo rais Shein amemteuwa mwakilishi wa jimbo la Welezo Hassan Khamis Hafidh kuwa Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda,wakati mwakilishi wa jimbo la Mtopepo dkt.Makame Ali Ussi anakuwa Naibu Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi.
Katika mabadiliko hayo hakuna Waziri aliyepoteza nafasi yake isipokuwa wamebadilisha Wizara tu na kuteuwa wajumbe wawili wa Baraza la Wawakilishi kuwa Manaibu Mawaziri.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu imesema mawaziri ambao hawakuguswa na mabadiliko hayo wataendelea kushikilia nyadhifa zao kama kawaida.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.




No comments:
Post a Comment