Kolimba ateta na Spika wa Bunge la EALA...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

NAIBU Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Susan Kolimba amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) Mhe. Martin Ngoga katika Ofisi za Wizara hiyo mjini Dodoma.

Katika mazungumzo yao  Dkt. Kolimba amemwahidi Spika wa EALA kuwa, Wizara na Serikali kwa ujumla itatoa ushirikiano wa hali ya juu kwa Bunge hilo katika utekelezaji wa majukumu yake ikiwa na lengo la kuboresha ushirikiano baina ya nchi wanachama wa EALA.

Kwa upande wake Spika wa EALA amesema kuwa, kwa sasa wamejipanga vizuri katika kuhakikisha wanadumisha ushirikiano na Mabunge ya Nchi wanachama na kutoa mrejesho kwa Nchi wanachama kuhusu masuala mbalimbali ya yanayojili katika Bunge hilo.

Spika Ngoga yupo Mkoani Dodoma ambapo Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki linaendelea na vikao vyake mjini humo ambavyo vimeanza April 9 na vinatarajiwa kumalizika April 28

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search