Mwili wa Mama Gambo kuzikwa Uru...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu, Arusha
Mama wa Mkuu wa mkoa Arusha, Mrisho Gambo anatarajiwa kuzikwa Uru mkoani Kilimanjaro baada ya mwili wake kurejeshwa nchini.
Katibu Tawala Mkoa Arusha, Richard Kwitega alisema hayo wakati akizungumza katika dua maalum leo, Aprili 14, iliyofanyika nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa.
Kwitega amesema "mwili wa marehemu Rehema Momburi, unatarajiwa kuwasili Jumanne kutoka nchini India,".
Kwa mujibu wa ratiba, mazishi yatafanyika Alhamisi ya wiki ijayo.
Viongozi mbalimbali wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa, umoja wafanyabiashara, wakurugenzi, mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema na viongozi wengine kadhaa walihudhuria.
No comments:
Post a Comment