Breakin News: Askari wa Bunge 'kumsindikiza Halima Mdee, Bulaya Kifungoni..' ni wale waliozembea agizo la Spika 'kumchomoa Mnyika Bungeni'

Mapya yameibuka sakata la Mbunge Mhe. Mnyika kutolewa kwa nguvu baada ya kukaidi agizo la Spika.

Askari walioagizwa kumtoa John Mnyika bungeni Ijumaa iliyopita, wamepangiwa vituo vingine vya kazi kwa kuchelewa kutekeleza agizo la Spika.

Akiongelea mtiririko baada ya hukumu ya mwaka mzima aliyopewa Mhe. Mdee na Ester Bulaya,.. Mhe. Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema aliwashangaa askari hao kwa jinsi walivyokuwa wanambeleza mbunge huyo wa Kibamba kutoka nje.

"Askari hawa wataendelea kuhamishwa mpaka pale tutakapowapata wanaofaa," amesema Ndugai.

pia sikiliza video hii Spika akizungumzia simu iliyopigwa na mama'ke na Mhe, Halima Mdee.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search