Hili ndio Gari atakalotumia Mkuu Mpya wa Mkoa Kilimanjaro Bi Anna Elisha Mghwira.. ambae ameapishwa Rasmi leo na Rais JPM - Ikulu Jijini Dar es Salaam!
Leo June 6, 2017 Ikulu Dar es salaam, limefanyika tukio kubwa na la kihistoria ambapo Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli amemuapisha Anna Mghwira, ambae alikuwa Kiongozi wa ngazi za juu na mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo, kuwa Mkuu mpya wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Katika siku za karibuni tokea jina la Mama Anna litajwe kushika nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Bw. Said Mecky Sadiq, kumekuwa na tashwishi kubwa kutoka washabiki na wanachama wa chama hicho kupitia mitandao ya kijamii, wakimtaka Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Bw. Zitto Kabwe kutoa tamko rasmi la chama hasa ikizingatiwa na tukio la hivi karibuni ambapo mfuasi mwengine na mshauri mkuu wa chama Profesa Kitila Mkumbo aliteuliwa kushika nafasi kubwa ya Ukatibu Mkuu katika Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Akijibu hoja hiyo juzi kupitia ukurasa wake wa Facebook, Mhe. Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, alisema kuwa maelezo rasmi yatatolewa baada ya suala hilo kujadiliwa katika ngazi ya Chama na Vikao husika.
Katika tukio hilo la kuapishwa kwa Bi Anna Mghwira, pia alipokea Ilani ya Chama cha Mapinduzi kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Bw. Rodrick Mpogolo, kama 'silaha muhimu' katika kuendesha majukumu yake. Itakumbukwa kuwa; kwa nafasi yake ya Ukuu wa Mkoa Kilimanjaro, Bi Mghwira pia anakuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa huo.
Matukio Blog kwa hisani kubwa ya Ikulu na Fullshangwe blog, inakuletea picha za matukio yote wakati wa Uapishwaji wa Bi Anna Mgwhira,.. Na tunaungana na Watanzania kumtakia Heri na Fanaka akielekea Kilimanjaro kuanza majukumu yake Mapya.
(PICHANI JUU, NI BIBI ANNA MGHWIRA AKIJIANDAA KUPANDA GARI RASMI LA MKUU WA MKOA KILIMANJARO: RC - KILI)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira akila kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakishuhudia tukio hilo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira akila kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira akisaini Hati ya Kiapo cha Udilifu kwa Viongozi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira akizungumza mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kumuapisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira Ikulu jijini Dar es Salaam.Kulia ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi ,Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na viongozi wengine Ikulu jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo akimkabidhi Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira huku Rais Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Salum Hapi pamoja na wakuuu wa Wilaya za Ubungo na Ilala wakipiga makofi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira akiwa amekaa kabla ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

No comments:
Post a Comment