Msiba wa Ndesamburo wazua mazito.. ASKOFU GWAJIMA amkemea RC Gambo hadharani.. amtaka 'aache kabisaa'

Hatimaye Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Kilimanjaro na Mbunge mstaafu wa jimbo la Moshi Mjini mzee Philemon Ndesamburo umeagwa jana Tar 5 Juni 2017 katika viwanja vya Majengo na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi na wageni kutoka sehemu mbali mbali pamoja na viongozi wa CHADEMA na vyama vyengine vya Upinzani, tayari kwa kuzikwa leo.


Katika Hafla hiyo, ambayo ilihudhuriwa pia na Viongozi mbali mbali wa Dini waliopata 'kutoa neno' alikuwepo pia Askofu wa kanisa la ufufuo na uzima Dr. Josephat Gwajima. Alipopata furasa ya kuzungumza kwenye mkusanyiko huo, Askofu Gwajima alianza na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kwa kukemea kile alichodai kuwa hakuwa sahihi kabisa kuzuia eneo lililokuwa limepangwa kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa marehemu.

bofya kitufe kumsikiliza askofu gwajima..#SHARE video kwa hisani ya Global Tv

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search