Nape aitaka serikali kukomesha vitendo vya kupigana risasi...Adai wahalifu wamo ndani ya serikali...#share
ALIYEKUWA Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Nape Nnauye ameitaka serikali kukomesha vitendo vya uhalifu vya kupiga watu lisasu na
kuwaonyesha silaha za moto ilikujitenga
nao.
Kauli hiyo imekuja siku
moja baada Mwanasheria Mkuu wa Chama Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Na Rais
wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kupigwa lisasi na watu wasiojulikana.
Akizungumza leo mjini
Dodoma Nape amedai kuwa wahalifu hao huenda wako ndani ya serikali na kusema kwamba
jambo hilo siyo la kulifumbia macho kwani hakuna mtu aliyeko salama.
“Wito kwa serikali ni
lazima jambo hilo walikomeshe ili serikali ijitenge na watu hao na inawezekana
wamo ndani ya serikali humo humo,”
“Lakini siamini kama
wanatumwa kufanya haya sasa kama watu wanafanya haya na wamo ndani na serikali
isipojitenga nao mana yake itakuwa sehemu yao na ikiwa sehemu yao itakuwa jambo
baya sana,” amesema Nape.
Akizungumzia kupigwa
risasi kwa Lissu, amesema tukio hilo ni moja tukio la hovyo kutokea nchini na alikumbusha kwamba
alipottolewa yeye silaha hadharani alisema kama mambo hayo hayatakomeshwa, ipo
siku mtu mwingine akapigwa risasi.
Nape amesema tukio hilo linashtua na linaumiza huku
akibainisha, Lissu ni mmoja wa watu waliolalamika kuwa amekuwa akifuatiliwa na watu
na kutaja namba na ragi ya gari inayomfuatilia
pamoja na idadi ya watu lakini cha kusikitisha ni kwamba hakuona hatua zilizochukuliwa
na kueleza kuwa vyombo husika walizpuuza taarifa hizo.
Ameongeza kuwa kwa mtindo huo huo jana alikuwa akifuatiliwa
nyuma na gari na waliokuwemo wakampiga risasi hivyo akaeleza kwamba jambo hilo
siyo dogo.
Hivyo uamuzi wa bunge
wa kulipeleka suala hilo kwenye kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama na kueleza
kuwa ni Imani yake kwamba baada ya hapo hatua zitachukuliwa.
Amesema kuwa wametoa
hatua zichukuliwe ilikukomesha jambo hilo kwani lisipo komeshwa litaendelea
kujenga chuki kati ya watanzania na serikali yao na kati ya watanzania na chama
kilichounda serikali.
Aidha amesema tukio
hilo linapeleka sura mbaya ya Tanzania duniani na watu kuweka dhana kwamba
wanaweza kuwa nchini na kupugwa risasi mchana kweupe na waliokupiga wakaitwa
wasio julikana.
Na Abraham Ntambara




No comments:
Post a Comment