Dk.Tizeba afukuza maofisa watatu...Soma habari kamili na Matukio360..#share
WAZIRI wa Kilimo Dk. Charles Tizeba amemuagiza Katibu m Mkuu wa wizara hiyo Methew
Mtigumwe kuwafukuza kazi Maofisa watatu wa Idara ya Maendeleo ya
Mazao katika sehemu ya pembejeo ambao wamebainika kuhusika na ukiukwaji wa
sheria, Kanuni na taratibu zilizowekwa.
Waziri wa kilimo Dk. Charles Tizeba (katikati) akisisitiza jambo Wakati wa Mkutano na waandishi wa habari Mjini Geita, Mwingine ni Naibu Waziri wa wizara hiyo Dk. Mary Mwanjelwa (Kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe.
Agizo hilo limetolewa leo na Waziri Tizeba akizungumza na waandishi
wa habari mjini Geita, amesema maofisa hao walikosa umakini katika usimamizi wa sheria ya ununuzi wa Umma.
“….ikiwemo kusababisha kuchapishwa kwa vocha za pembejeo
zenye thamani ya Tshs 78,054,970,000 ambazo ni zaidi ya bajeti halisi
iliyotengwa kwa ajili ya ruzuku ya pembejeo kwa kiasi cha Tshs 42,587,419,200,”
amesema Tizeba.
Maafisa waliofukuzwa kazi ni Shenal S. Nyoni aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi
wa kitengo cha pembejeo, Michael G. Mayabu aliyekuwa Afisa kilimo Daraja la I na
Bw Michael G. Mayabu na Franks F. Kamhabwa.
Aidha Tizeba ametoa agizo hilo baada ya kupitia taarifa ya
waraka wa mkakati wa utekelezaji na usimamizi wa utoaji wa Ruzuku za pembejeo
za kilimo kwa wakulima kwa kutumia vocha wa mwaka 2015/2016 ambapo pamoja na
mambo mengine uliainisha utaratibu wa usimamizi wa zoezi la utopaji wa ruzuku
ambao ulilenga kuleta ufanisi katika utekelezaji wake.
Katika hatua nyingine Tizeba waziri huyo amemuagiza katibu
Mkuu Mtigumwe kuwasimamisha kazi watumishi wengine watatu ambao ni Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Mazao Twahir S. Nzallawahe,
Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi Burhan A. Shaban na Kaimu Mkurugenzi
Msaidizi wa Kitengo cha pembejeo Canuth
Komba.
Hatua hiyo imekuja kutokana na uzembe ambao ungeweza
kusababisha upotevu wa zaidi ya sh. 29,977,114,700 kwa mwaka wa fedha wa 2015/2016 ambapo serikali ilitenga
sh. 35,467,550,800 kwa ajili ya pembejeo za kilimo na mara baada ya zoezi la
utoaji ruzuku ilibainika kuwa deni lililowasilishwa serikalini na mawakala
ilikuwa ni kiasi cha sh. 65,444,665,500.
Sambamba na hayo Tizeba ameviomba vyombo vya dola kuchunguza
zaidi na kuchukua hatua stahiki za kisheria dhidi ya watumishi na watu wote
waliohusika katika ngazi za halmashauri na mawakala wote waliofanya udanganyifu
kwa lengo la kuisababishia serikali hasara.
Waziri Tizeba (katikati) akisisitiza jambo Wakati wa Mkutano na waandishi wa habari Mjini Geita, Mwingine ni Naibu Waziri Mhe Dk. Mwanjelwa (Kushoto) na Katibu Mkuu Wizara Methew Mtigumwe.
Waziri Tizeba akitafakari jambo mara baada ya kuzungumza na vyombo vya habari Mjini Geita



No comments:
Post a Comment