Mkuchika: Kuna rushwa kubwa Sekretarieti ya Ajira...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Salha Mohamed
WAZIRI wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimanti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amesema
Sekretarieti ya ajira inachangamoto kubwa ya kukabiliana na vitendo vya rushwa.
Waziri George Mkuchika (katikati) akisisitiza jambo
wakati akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Ajira jijini Dar es Salaam.
Amesema hayo leo jijini
Dar es Salaam katika ziara yake ya kuangalia utekelezaji wa majukumu ya
Sekretarieti ya Ajira.
Mkuchika amesema
wizara yake ndiyo inayofuata sheria
hivyo watumishi wake wanapaswa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu
na kuwa ataraji kusikia malalamiko kutoka kwa wananchi.
"Hakuna mahala
penye ushawishi na kupewa rushwa kama hapa Sekretarieti ya Ajira, muwe makini
na maadili kwa kutenda haki kwa wenye sifa kupata kazi, usiombe faili liletwe
kama kunamtumishi kapokea rushwa, mjiepushe na rushwa na mtende
haki,"amesema.
Pia amesema Serikali itarekebisha
sheria za uajiri kwa watumishi wote nchini kupitia Sekretarieti ya ajira.
Hatua hiyo inatokana na sheria iliyofanyiwa marekebisho ya sheria
ya Utumishi wa Umma Na 8 ya mwaka 2012 yaliyofanywa kupitia sheria Na 2 ya mwaka
2013 kuwa na mapungufu.
Mkuchika amesema
sheria hiyo ya uajiri inamapungufu katika kuajiri baadhi ya watumishi katika
kada mbalimbali kwani wapo wanaoajiri moja kwa moja bila kupitia katika sekretarienti hiyo.
"Kuna mapungufu
ya Sheria, naahidi katika kipindi changu cha uongozi...tutayaangalia Bungeni
lakini kadri tunavyoendelea zinajitokeza changamoto mbalimbali."amesema.
Kwa upande wake
Katibu Sekretarieti ya Ajira Xavier Daudi amesema wamepunguza watumishi wa
vyeti vya kughushi katika mchakato wa ajira serikalini kutokana na uhakiki
wanaofanya .
"Haina budi
kuwezeshwa katika rasilimali fedha kwa kupitia bajeti inayokidhi mahitaji ili kuongeza
weledi na kutumia mbinu na mifumo mipya na ya kisasa kwenye mifumo yake ili
kupata rasilimali watu waliokidhi mahitaji ya sasa,"amesema.
Waziri George Mkuchika akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Sekretarieti ya Ajira Jijini Dar es Salaam.





No comments:
Post a Comment