Mhasibu wa ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji atuhumiwa kuchota mamilioni..Apandishwa kizimbani..Soma habari kamili na Matukio360..#share
JOYCE Moshi(56) ambaye ni Mhasibu wa Ubalozi wa
Tanzania nchini Msumbiji, amepandishwa
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka tisa ikiwamo la
utakatishaji fedha wa dola za Marekani 150,000.
Miongoni mwa mashtaka mengine yanayomkabili ni
kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi, wizi akiwa mtumishi wa umma na
utakatishaji wa fedha.
Wakili wa Serikali, Wankyo Simon amemsomea mashtaka yanayomkabili mshtakiwa huyo leo
mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.
Akisoma mashtaka hayo, Wakili wa Wankyo amedai Oktoba 25, 2016 katika Ofisi za Ubalozi wa
Tanzania zilizopo Maputo nchini Msumbiji,
mshtakiwa huyo alighushi barua ya Oktoba 25, 2016.
Akijaribu
kuonesha kuwa ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Maputo Msumbiji
umeilekeza Benki ya Millennium BIM ya Maputo, kuhamisha kiasi cha dola za
Marekani 10,000 kutoka kwenye akaunti namba 79667362 kwenda akaunti namba
182283177 inayomilikiwa na Mushi na kwambq akaunti hizo zote zipo kwenye benki hiyo iliyopo katika tawi la
Julius Nyerere Maputo, wakati akijua si kweli.
Mshitakiwa huyo anadaiwa kuwa Februari 10, 2017 katika
ofisi za Ubalozi Maputo Msumbiji, mshitakiwa huyo alighushi barua ya Februari 10, 2017 alionyesha kuwa ubalozi huo umeielekeza Benki ya ya
Millennium BIM ya Maputo, kuhamisha dola za Marekani 10,000 kutoka akaunti
namba 79667362 kwenda akaunti namba 182283177 inayomilikiwa na Moshi.
Mshitakiwa huyo anadaiwa kuwa Aprili 12, 2017 katika Ofisi za Ubalozi wa
Tanzania Maputo nchini Msumbiji,
alighushi barua ya Aprili 12, 2017 akijaribu kuonesha kuwa ubalozi huo
umeielekeza Benki ya Millennium BIM ya
Maputo, kuhamisha dola za Marekani 40,000 kutoka akaunti namba 79667362 kwenda
akaunti namba 182283177.
Oktoba 25, 2016 mshitakiwa huyo katika Benki ya Millennium BIM iliyopo tawi
la Julius Nyerere Maputo nchini
Msumbiji, aliwasilisha kwenye benki hiyo nyaraka za kughushi ambayo ni barua ya
Oktoba 25, 2016 akionesha kuwa Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji umeelekeza
benki hiyo kuamisha dola za Marekani 10,000 kutoka kwenye akaunti ya benki hiyo
kwenda kwenye akaunti inayomilikiwa na mshitakiwa huyo.
Wankyo aliendelea kudai kuwa Februari 10, 2017 katika
benki hiyo, Moshi alitoa nyaraka za uongo kuonesha kwamba Ubalozi umeelekeza
kuamisha dola za Marekani 10,000 kwenda kwenye akaunti ya Mushi.
Ili endelea kudai wa kuwac Aprili 12, 2017 katika
maeneo ya benki hiyo mshtakiwa huyo aliwasilisha barua ya Aprili 12, 2017
kuonesha kuwa ubalozi umeelekeza kuamisha dola za Marekani 40,000 kwenda kwenye
akaunti ya Moshi.
Wankyo alidai mshitakiwa huyo katika tarehe tofauti
kati ya Oktoba 25,2016 na Aprili 12, 2017
akiwa mtumishi wa umma kama
Mhasibu wa Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji, aliiba dola za Marekani 150,000
mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Inadaiwa kati ya Oktoba 25, 2016 na Aprili 12, 2017
katika ofisi za ubalozi huo, Moshi alijipatia dola za Marekani 150,000.
Wanadaiwa kuwa,
kati ya Oktoba 25, 2016 na Aprili 12, 2017 katika ofisi za Ubalozi wa
Tanzania uliopo Maputo nchini Msumbiji na Benki ya Millenium BIM tawi la Julius
Nyerere Maputo, alijipatia dola za Marekani 150,000 wakati akijua fedha hizo ni
zao la kughushi.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, mshitakiwa huyo
alikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado
haujakamilika na kwamba tarehe ijayo wataeleza
hatua zilizofikiwa.
Wakili wa utetezi, Jebra Kambore aliomba upande wa
mashtaka wajitahidi kukamilisha upelelezi kwa wakati.
Hakimu Shaidi aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 31,
2017 kwa ajili ya kutajwa. Mshitakiwa alipelekwa Mahabusu.




No comments:
Post a Comment