Auwawa akituhumiwa kuiba kuku ...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwajuma Juma, Zanzibar
WATU wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti Visiwani Zanzibar likiwamo la wizi wa kuku.
Kamanda Hassan Bashir
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa mjini Magharibi, Hassan Nassir amemtaja marehemu huyo kuwa ni Ali Simai Khamis (28) mkazi wa Kama ambaye alifariki dunia kutokana na majeraha baada kupigwa na watu wasiojuulikana.
Amesema marehemu alichomwa na kitu chenye ncha kali mguu wa kushoto na kushambuliwa sehemu mbali mbali za mwili wake kwa mawe na marungu pamoja na kufungwa kamba mikononi.
Kwa mujibu wa kamanda Nassir sababu ya shambulio hilo ni kuiba kuku na kwamba watu wawili wamekamatwa na uchunguzi unaendelea. Tukio hilo limetokea Januari 16, 2018
Mwingine aliyefariki ni Majaliwa Hussein (34) mkazi wa Chalinze
Dar es Salaam ambaye alikutwa amekufa Forodhani nyuma ya Hoteli
ya Tembo, alipokuwa akiogelea na wenzake.
Amesema mwili wa marehemu ulifikishwa katika Hospitali ya Mnazi
mmoja kwa uchunguzi na kukabidhiwa ndugu zake kwa mazishi, tukio
lilitokea Januari 19 mwaka huu majira ya saa 9:00 za Alasir.
No comments:
Post a Comment