Onesho chimbuko la binadamu kuonyeshwa bure DSM...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
MAKUMBUSHO ya Taifa
kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Ubalozi wa Hispania nchini
imeandaa onesho la chimbuko la binadamu barani Afrika pamoja na semina. Litafanyika kesho jioni Januari 23, 2018.
Mkurugenzi Mkuu wa makumbusho ya taifa, Profesa Audax Mabulla akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Profesa
Audax Mabulla alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es
Salaam, amesam semina na onesho hilo ni matokeo ya tafiti mbalimbali
zinazofanyika bonde la Olduvai na Laetoli na hifadhi ya mamlaka ya Ngorongoro.
“Onesho hili litafunguliwa rasmi na Dk.Hamis
Kigwangalla, waziri wa maliasili na utalii kesho saa 11 jioni hapa Makumbusho
ya Taifa,” amesema Prof. Mabulla.
Amesema onesho limegawanyika katika sehemu nne zanazowiana.
Sehemu ya kwanza litahusu ushahidi wa nyayo za binadamu zilizogunduliwa huko Laetoli
mwaka 1978 na mtafiti Dk. Mary Leakey.
Sehemu ya pili itahusu hadithi ya kusisimua ya kuwa binadamu
(Genus Homo) ambapo kuna masalia ya binadamu Zinjanthropus au Paranthropus na
Homo habilis, zana za mawe za mwanzo (Oldwan) zilizotumika katika kujipatia
chakula na ushahidi wa kale wa ulaji wa nyama katika historia ya mabadiliko ya
binadamu, takribani miaka milioni 2 iliyopita.
Amesema sehemu ya tatu itahusu maisha ya jamii ya Homo
erectus. Jamii hii inafanana zaidi na binadamu wawa sasa kuliko jamii zilizotangulia.
Na sehemu ya nne amesema itaonesha kipindi cha mwanzo cha
binadamu wa sasa (Homo sapiens) walioanza kutokea Afrika miaka laki 2
iliyopita.
Profesa Mabulla amewaomba wananchi na wadau mbali mbali
kujitokeza katika onesho na semina na kwamba itakuwa bure.
No comments:
Post a Comment