Serikali yaokoa bilioni moja....soma habari kamili na matukio360
Na mwandishi wetu, Dar es salaam
SERIKALI imeokoa zaidi ya sh bilioni moja kukarabati magari 11 ya Vyombo vya ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Polisi, Magereza na Jeshi la Wananchi baada ya kukarabatiwa na Kampuni ya Dar Coach Ltd bure.
Paul Makonda akikagua moja ya magari yanayoendelea kukarabatiwa
Hayo yamebainishwa Dar es Salaam leo wakati Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa mabasi hayo 11 yanayotarajiwa kumalizika ukarabati
mwishoni mwa Januari, 2018.
Magari hayo ni yale yaliyopelekwa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani yakiwa Chakavu(Screpa) ambapo sasa yapo katika hatua ya mwisho kukamilika kwa kufungwa vifaa vya kisasa ikiwemo AC, Chaji ya Simu, TV, Viti, Bodi mpya, Taa, Side mirrors, Tairi huku baadhi zikiwekewa Vyoo vya Ndani.
Kutokana na ukarabati huo Makonda ameridhishwa na kasi ya ukarabati huo ambapo ameshukuru kiwanda cha Dar Coach Ltd kwa uzalendo wa kujitolea kukarabati Magari hayo.
Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama walioambatana na Makonda akiwemo Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Mkoa huo, Lazaro Mambosasa, Mkuu wa Jeshi la Magereza (DCP),Agustin Mboje na Kaimu Mkuu wa Usafirishaji (JWTZ),Canal Benjamin Kisinda wamempongeza Makonda kwa ubunifu anaoufanya.
Wamesema Magari hayo yatasaidia kuimarisha ulinzi na usalama pamoja na askari kufanya kazi katika mazingira mazuri.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Dar Coach Ltd, Manmeet Lal amemhakikishia Makonda kuwa magari 5 kati ya 11 yatakabidhiwa mwishoni mwa mwezi huu.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment