Polisi wampiga 'stop' Zitto Kabwe...soma habari kamili na matukio....#share
Na Mwandisshi Wetu,
JESHI la polisi mkoani Kigoma limezuia mkutano wa hadhara wa mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe.
Zitto Kabwe.
Kwa mujibu wa Zitto kupitia ukurasa wake wa Facebook amesema zuio hilo ni kinyume na sheria ya Bunge ya mwaka 1988. Sheria Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge inalazimisha ( kwa kutumia neno SHALL ) Mbunge kufanya mkutano kwenye jimbo lake bila vikwazo.
"Mimi sitaki kuwapa polisi sifa ya kupambana nasi. Tumeahirisha mkutano mpaka siku ya jumamosi Lakini tumewaandikia barua rasmi kuwa sheria waliyonukuu sio sheria halali na haihusiani na mikutano ya Mbunge kwenye jimbo lake la Uchaguzi. Sheria wanayopaswa kunukuu ni sheria namba 3 ya mwaka 1988 kifungu cha 4(1)," amesema Zitto.
"Nitamwandikia mheshimiwa Spika rasmi kuhusu suala hili ili lisifanyike kwa Mbunge mwengine yeyote," ameongeza.
Taarifa ya polisi
No comments:
Post a Comment