Tetesi za soka Ulaya leo Alhamisi.... soma habari kamili na matukio360...#share
Na mashirika ya kimataifa
WINGA wa Chelsea Mbrazil, Willian (29) anaweza kuiacha timu hiyo katikati ya mwaka na huenda akujiunga na timu ya AC Milan au Manchester United (Star)
Willian
WINGA wa Chelsea Mbrazil, Willian (29) anaweza kuiacha timu hiyo katikati ya mwaka na huenda akujiunga na timu ya AC Milan au Manchester United (Star)
Willian
Manchester United wameongeza muda ya mikataba ya mchezaji Ashley Young, 32, na Daley Blind, 27, na ule wa mlinda mlango Sam Johnstone, 24
Mashetani hao wekundu wana mipango wa kumuacha kiungo Marouane Fellaini, 30, na Michael Carrick, 36, na mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic ambao watakuwa huru kuondoka na kwa usajili huru majira ya joto.
Manchester United wataachana na mpango wa kuupanua uwanja wa Old Trafford mwaka huu na kujikita zaidi katika kumuunga mkono Jose Mourinho katika kutafuta wachezaji.(Mail)
Uongozi wa timu ya Arsenal wamemgeukia meneja wao, Arsene Wenger na kuanza kuorodhesha majina mbadala kuchukua nafasi yake.
Hata hivyo Wenger anasema "atapindua dunia chini juu" ilikubaki kama meneja wa Arsenal
Kibarua chake kimewekwa matatani wakati alipokataa kuthibitisha kama ataendelea na mkataba wake unaoisha 2019. (Mirror)
Aliyekuwa rais wa timu ya Barcelona Joan Laporta, amesema anawahimiza Arsenal kumfikiria Thierry Henry kama mbadala wa Wenger.(Telegraph)
West Ham iko tayari kumsiani mlinzi wa Ireland Kaskazini Jonny Evans, 30, kwa paundi milioni tatu kutoka kwa West Brom ikifika mwisho wa msimu. (Birmingham Mail)
Kiungo wa Arsenal na timu ya England, Jack Wilshere, 26 anasema atatoka kwenye klabu hiyo kati kati ya mwaka huu, wasipo mpatia mkataba bora zaidi. (Sun)




No comments:
Post a Comment