Wanawake ACT-Wazalendo watoa neno kwa serikali...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara,
Dar es Salaam
CHAMA cha ACT-Wazalendo
kupitia Ngome ya Wanawake kimeitaka serikali kuacha ukandamizaji wa Demokrasia
na haki za binadamu.
Msimamo huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti Ngome ya Wanawake Taifa wa chama hicho, Chiku Abwao alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali na
mwenendo wa siasa na haki za binadamu nchini.
“Tunaitaka serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Rais Magufuli iache ukandamizaji wa
demokrasia na haki za binadamu. Ni muhimu nchi iendeshwe kwa kufuata misingi ya
haki na utu,” amesema Abwao.
Amesema nchi inayominya
haki haki dhidi ya wananchi wake huzaa taharuki, hofu na hali ya unyonge hivyo
ni rahisi kutumbukia katika machafuko kwa kuwa wananchi watachoka kukandamizwa,
kubuluzwa, kunyanyaswa na kuonewa.
Pia amelitaka jeshi la
polisi kuacha kutumika kukandamiza haki za raia kwani wajibu wake ni kulinda
mali na haki zao.
Amesema tangu kuingia kwa serikali ya awamu ya tano matukio mbalimbali ya kusikitisha yameongezeka kinyume na utamaduni mzuri ambao nchi ilikuwa
ikiujenga.
“Matukio ya watu
kupotea katika mazingira ya kutatanisha, kutekwa na kuteswahasa na jeshi la
polisi sasa yamekuwa sehemu ya maisha ya watanzania, hali hii haikubaliki na
tumeona tujitokeze na kuchukua wajibu wa kusema na kukemea ili kulinusuru taifa
na hatari inayolinyemelea,” amesema.
Akizungumzia kuhusu
mfumo wa vyama vingi, ameitaka serikali kutenda haki kwa vyama vya siasa
kufanya kazi zao kwa uhuru ni takwa la kikatiba na si hisani ya watawala.
Pamoja na mambo mengine ngome hiyo imetoa mapendekezo sita, kurejesha mchakato wa
katiba mpya kwani ndiyo itakuwa jibu la msingi kwa changamoto zinazolikabili
taifa.
Mengine, imeitaka
serikali kuacha kujenga mazingira kandamizi na hofu, kutishia wananchi
(wanyonge), kuwanyanyasa kiasi kwamba wanashindwa kupumua na kufaidi utanzania
uliojengwa katika misingi ya utu na heshima kwa binadamu wote bila kujali
vyama, dini na ukabila.
Pia imetaka kuundwa kwa
tume huru ya uchaguzi ili kusaidia kufanya uchaguzi huru na wa haki.




No comments:
Post a Comment