Anaandika Emmauel dk(mwanaharakati msomi wa maswala ya fursa nchini): kwa nini Fursa ya kufanya ujasiriamali ni muhimu!!


KWANINI FURSA YA KUFANYA UJASIRIAMALI NI MUHIMU

Kumekuwepo na wimbi la watu wengi sana kufanya uamuzi wa kuingia kwenye ujasiriamali…kuachana na ajira zao za serikali au mashirika binafsi walioajiriwa. Wengine huamua kufanya kazi za kuajiriwa na ujasiriamali kwa wakati mmoja, wengine huamua kuwa wajasiriamali kwa asilimia 100%.


Je, ni kitu gani kiwafanya watatu wengi kuingia kwenye ujasiriamali?

Sababu ya kwanza wengi wao WAMEAMUA KUWA MILIONEA. WAMEAMUA KUWA MILIONEA WA DOLA. Maamuzi haya hufikiwa na kuchagiwa na tafiti zinazoonesha ni ngumu mno kwa mwajiriwa wa kawaida kuwa milionea wa dola labda awe mla rushwa au mwizi katika maisha ya kawaida. Na hili linatokana na mfumo wa kibepari unavyoendeshwa na falsafa nyuma ya mishahara na inapangwaje.

Ubepari ni nini katika karne hii? Kwa wale ambao mmesoma masomo ya sayansi ya jamii mnamtambua vyema Karl Marx. Marx aliubainisha vyema mfumo huu kwa kuonesha kuwa ni wa kinyonanyaji na una matabaka makuu mawili. Moja ni la wachache, mabepari wenye mtaji yaani Capitalists, na kundi la wengi ni wanyonywaji ambao ni wafanyakazi yaani Proletariats. Sifa kubwa ya Proletariats ni kuwa wanamiliki nguvu ya kazi na hawana chochote cha kupoteza (Proletariats have nothing to loose than the chains). Hivyo ukimfukuza Proletariat unakuwa kama vile umemsaidia kuondokana na minyororo ya unyonywaji katika mfumo wa ubepari. Na mwenye cha kupoteza ni mwenye mtaji, Capitalists. Ndio maana katika kipindi cha mapinduzi ya viwanda, migomo kama ile ya Luddites ilitoa hasara kubwa kwa wenye mitaji. Kitu kikubwa ni kwamba mfumo huu ambao Marx anaungumzia ni ule wa 1850s.

Ubepari wa sasahivi 2000s upoje? Je, ni nani ana cha kupoteza kati ya Capitalist na Proletariat? In my own words, Capitalism is the most sophisticated slavery in the modern era. Kipindi cha utumwa (slave mode of production), watumwa walikamatwa, kuteswa, kufanyishwa kazi kwa nguvu bila malipo nk. Sasahivi, baada ya 1850s ambapo Capitalists had something to loose wakaona ni vyema kufanya modification ya capitalism of 1850s to modern day slavery in 2000s.

Bepari anachofanya sasahivi ni kukuwekea mazingira uchukue mkopo wa gari, nyumba na mahitaji mengine. Bepari anakuwekea mazingira umpeleke motto kwenye shule binafsi za ghali kuendana na "hadhi" yako. Hii ni mbinu. Unapokuwa na madeni kama haya, maana yake unakuwa mtumwa kwenye kazi yako, mtumwa kwa mwajiri wako. Itakulazimu ujifunge minyororo ya utumwa mwenyewe sasahivi bila kulazimishwa. Sasahivi itakulazimu uweke alarm clock, uamke usiku mnene saa kumi asubuhi kuwahi kazini kukwepa foleni. SASAHIVI UNA CHA KUPOTEZA, tena kitu kikubwa sana. Huwezi kugoma kazini. Huwezi kuacha kazi. Unamilikiwa na bepari. Ukiacha kazi au kugoma maana yake utanyang'anywa gari, utafukuzwa kwenye nyumba ya mkopo, mtoto wako kwenye shule binafsi ya kimataifa atafukuzwa toka Saint Mary's, Mazinde, Feza nk na kuhamia Saint Kayumba, hapo utakuwa umeibua mgogoro mkubwa sana na vita kati yako na mtoto wako. Bepari sasahivi anaweka utaratibu wa Family Day. Usishangilie siku hii, kwani ni siku ambayo mtoto wako atakutana na mtoto wa CEO wako na kuongea maisha ya shule zao. Utashawishiwa umpeleke mtoto wako shule nzuri kama ya CEO wako, wanakuweka kwenye madeni ili waku-own na uwe na nidhamu kuogopa kupoteza sana ukiachishwa kazi.

Falsafa ya mshahara ni nzito mno kwenye mfumo huu wa kibepari. Unapopewa mshahara, mshahara umekuwa designed kuhakikisha unatumika na kuisha kabla ya mwisho wa mwezi, na ukiwa mjanja basi mshahara usizidi tarehe 30 ya mwezi huo. Maana mshahara ukiwa mkubwa na kubakia utakuwa na kiburi cha hata kutokwenda kazini tarehe 2 ya mwezi unaofuata. Hivyo mshahara hata kama unapanda, upo calculated na hali ya maisha ya wakati husika. Lakini pia mshahara hata kama ukipanda, kisaikolojia na maisha yako yatabadilika kuongeza matumizi. Hivyo mshahara hata uwe milioni 10 kwa mwezi utaisha ndani ya siku 30 za mwezi husika. Jambo la kutafakari unafanyakazi kwa mwezi unapata Laki 700,000 makato (PAY, NHIF, NSSF, Board ya Mikopo) takehome 550,000 matumizi (kodi 100,000, Usafiri 100,000, Chakula 200,000, Mavazi 50,000, umeme na maji 50,000, mawasiliano 20,000, dharula 20,000) Kazi ni kwako utakuwa milionea lini?

Kutokana na hali hii, umamuzi wa kufanya upo mikononi mwako. Aidha, kuchague kuwa mnyonywaji, proletariat ambaye katika karne hii una cha kupoteza kwa kuwa mtumwa. Au uchague kuwa bepari, mwenye mtaji na kufanya maisha yako bila kuhofia kupoteza dhidi ya utumwa wa kisasa. Amua kuwa BEPARI. Amua kupinga kuwa slave in this sophisticated slave mode of production (other people call it Capitalism). Hivyo, YOU HAVE NO OTHER CHOICE BUT TO BE AN ENTERPRENEUR AND OBVIOUS MILLIONIRE.

Je, umeamua kuwa mjasiriamali kwa sababu gani? Kipi kimekusukuma kuwa mjasiriamali?

NB: Tafadhali, baada ya kumaliza kusoma, share na watumie ndugu, jamaa, marafiki na wengineo wenye kupenda kujua mambo ya ujasiriamali.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search