Picha 10: Maajabu ya 'Beach Maiti' Bwawa kubwa lililohama usiku wa manane kutokana na mafuriko. Pata picha na video ya muonekano mpya wa eneo la 'Bwawa' hili na sasa ni Crater kuubwa ya kutalii

MPENDWA MSOMAJI: Matukio Blog ni mkaazi wa eneo la Kata ya Chamazi Mbagala Jijini Dar es Salaam; linakopatikana bwawa maarufu la ‘kwa Mzala’.. bwawa maarufu kwa shuguli za Uvuvi wa Samaki aina ya Kambale, Perege, Mkunga, na aina nyenginezo nyingi na vijana wengi humiminika eneo hili kwa ajili ya kujipatia kipato kutokana na uvuvi na uuzaji wa Samaki.
Pia Bwawa hili limehusishwa na mambo ya kiimani zaidi, na wenyeji wa huku wamelibatiza bwawa hili na sasa linajulikana sana kama ‘Beach Maiti’ kutokana na kuwa hatarishi kwa maisha ya watu.. na imani inalihusisha bwawa hili na kiumbe aitwae Chunusi ambae ambae husemekana na kuondoka na roho ya mtu mmoja kila mwaka.
Ndugu msomaji wa mkasa huu vuta hisia,.. bwawa hili ni kubwa sana na lenye kina kikubwa cha maji. Bwawa hili lina urefu usiopongua mita 300 na upana usiopongua mita 200, na sasa imebaki simulizi tuu.. Bwawa halipo tena eneo husika.
Mkasa mzima umetokea juzi alfajiri ya kuamkia Alhamis tarehe 12/05/2017 wakati mvua zikiendelea bwawa likatafuta njia kwa kuvunja kingo zake na kutoweka ‘mazima’!!
Nyumba zisizopungua 20 na miti mikubwa aina ya miembe na minazi nayo ikapata njia na kutoeka na sasa eneo hili limekuwa sehemu ya Crater kuubwa inayovutia watu kwa mamia wanaofika kujionea kilichotokea na mandhari hii mpya..
Kwa picha zaidi na video tuwasiliane kwa namba: 0715722673 na 0786722673
Endelea kufuatilia blog yako yako ya Matukio na kuiunga mkono kwa kugonga ‘like’ halafu ‘share’ www.tanzaniampyamatukio.blogspot.com

Nyumba hii ilibaki nusu mmiliki asijue la kufanya
Nimekuekea Video ya eneo husika, vuta picha hili eneo lilijulikana kwa jina la utani la 'Beach Maiti' kutokana na kuwa maji mengi msimu wote na kuwa hatarishi kwa maisha ya watoto wanaoshinda humo wakivua samaki.. ni maajabu hili bwawa limehama bila kubakia hata tone la maji.. ikikupendeza pata mda utembelee mahala hapa si mkasa wa kusimuliwa:
https://goo.gl/photos/PK3arwFiF7Lc5H8g8


Sasa imekuwa Crater baada badala ya bwawa maarufu la kwa 'Mzala'

Baadhi ya majumba yaliyosalia baada nyumba nyengine nyingi kusombwa na maji

Maskini.. Watumiaji wa njia hii wakishangaa kukuta njia yao waliyoizoea haipo tena

Kabla tukio eneo lote hili lilikuwa katika usawa mmoja !

Wananchi wa kwa Mzala na wa maeneo mbali mbali walimiminika kwa wingi kushuhudia yaliyojiri

Njia ya maji ya sasa baada ya bwawa kuvunja kingo na maji yote kuvuja

Eneo hili zamani lilikuwa bwawa kubwa la uvuvi wa samaki aina mbali mbali

Eneo lililosombwa na maji ambalo awali yalikuwa makazi ya watu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search