LUKUVI Kweli Shujaa!! #SHARE halafu uone alichokifanya Msibani kwa Mzee Ndesamburo !

Katika hali iliyoonyesha ukomavu alionao Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Lukuvi, leo alikuwa kivutio kikubwa na faraja kwa wafiwa alipojitokeza na kuwa mstari wa mbele katika uagwaji na hatimaye Mazishi ya 'Gwijji wa SIASA' Tanzania Mzee Philemon Ndesamburo .

Akionekana kiongozi pekee wa ngazi ya juu kutoka upande wa Serikali, Mhe. Lukuvi aliejawa Na majonzi na simanzi usoni mwake, na kuonekana wazi kuguswa na msiba huo alijitokeza na kushiriki 'mwanzo mwisho' kutoa heshima za mwisho kabla kupata fursa ya kumwaga mashada ya Maua juu ya Kaburi la Mwendazake.. Mzee Ndesamburo... huku akiwa bega kwa bega na wenyeji wake viongozi kutoka kambi ya Upinzani akiwemo Mhe. James Mbatia...

Matukio blog tuliahidi kuwaletea tukio zima la Kumuenzi Mzee Ndesamburo, tumekuwekea picha ya Mhe Lukuvi akishiriki kikamilifu katika msiba huu mkumbwa...
Endelea kuwa nasi kupitia kiunganishi chako: www.matukiotza.blogspot.com





Bofya 'play' umsikilize Mhe. Lukuvi akiongea machache.. 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search