Fursa: Watanzania wametakiwa kuchangamkia fursa kibiashara kwa kutumia kikoa (Domain) cha .tz. badala ya .com, yahoo, gmail.....#share
WATANZANIA wametakiwa
kutumia kikoa (domain) cha .tz. huku akiwataka kuachana na vikoa vingine vya
mataifa mengine kama vya .com, Hotmail, Gmail, yahoo na nyinginezo ili
kunufaika katika shughuli za biashara.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani wakati wa ufunguzi wa
mkutano ambao unajadili jinsi ya kushirikiana kukuza matumizi ya vikoa kwa
wananchi kwa nchi mbalimbali ambazo zimeshiriki mkutano huo.
Amesema kuwa kwa kutumia kikoa
hicho itakuwa rahisi kwa mfanyabiashara,
kufanya biashara kwa urahisi kwani anapofanya mawasiliano na wabia wake
atatambulika vyema pasipo kutiliwa shaka kutokana na utambulisho kuwa yeye ni
mtanzania.
Aidha Naibu Waziri huyo amesema matumizi ya Watanzania
wanaotumia kikao cha .tz ni ndogo kulinganisha na idadi ya watumiaji wa
mitandao nchini hivyo wabadilike kwani kwa kutumia vikoa tofauti na .tz
wanazifaidisha nchi zinamiliki hivyo vikoa.
“Sisi Tanzania tupo nyuma sana
inawezekana ni kwasababu mambo mengi hatuelewi tumezoea kutumia .com, hotmail,
gmail lakini hizo sio zetu ni za Wamarekani au Waingereza ni wakati umefika
sasa na sisi tuna uwezo wa kutengeneza rajisi yetu,
“Tuwahamasishe Watanzania kuwa
waachane na matumizi ya .com, yahoo, hotmail na kadhalika sababu tunawanufaisha
mataifa ya nje, katika kila huduma unayotumia katika mitandao ile mataifa ya
nje ndiyo yananufaika,” amesema Mhandisi Ngonyani na kuongeza.
“Faida kubwa kwa kutumia kikoa cha
Tanzania ni kwamba mtu akiwa Australia anawasiliana na wewe akiona unatumia .tz
anajua upo Tanzania lakini ukitumia .com hawezi kujua upo wapi, ukiwa unaagiza
vitu kutoka nje ukitumia .tz inakusaidia sana kukutambulisha kuwa wewe ni
Mtanzania, inakupa uaminifu, inampa mtu imani kuwa huyu ni mtu sahihi na yupo
Tanzania.”
Nae Makamu wa Rais wa AfTLD, Alli Hadji Mmadi alisema
matumizi ya kikoa kwa Afrika bado ni madogo kulinganisha na idadi ya watu
waliopo na hivyo kuwataka watu wote ambao wanatumia mitandao kuhakikisha
wanatumia kikao cha .tz.
“Kwanini usitumie kikao cha .tz na
wakati kinakutambulisha wewe unatokea sehemu gani, matumizi ya vikoa Afrika
bado ni madogo sana na hilo ni changamoto, kati ya watu bilioni ni watu milioni
2.9 tu ndiyo wanatumia vikoa vya nchi zao, tuna kazi ya kuhakikisha idadi
inaongezeka,” amsema
Mmadi.
Kwa upande wa Mkurugenzi mtendaji wa .tz Registry, Abibu
Ntahigiye amesema huo ni mkutano wa tano kufanyika na kupitia mkutano huo
wataweza kuzungumza ni namna gani wanaongeza idadi ya watumiaji wa vikoa vya
Afrika.
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment