RONALDO DE LIMA NA FIGO WASHUHUDIA MESSI AKIINYONGA MADRID DIMBANI EL CLASICO
FC Barcelona walisafiri kuelekea Madrid tayari wakiwa
wanamkosa mchezaji wao wa kimataifa wa Brazil Neymar kutokana na kutumikia
adhabu ya kufungiwa mechi tatu, licha ya kumkosa Neymar safu ya ushambuliaji ya
Barcelona bado ilikuwa imara na kupelekea kupata ushindi wa magoli 3-2.
Mshambuliaji wa
Barcelona na timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi ndio ameonekana
kuwa hatari zaidi kwa kumsababishia Sergio Ramos kupata kadi nyekundu ya 22
katika historia yake ya soka kutoka na kumchezea Lionel Messi faulo dakika ya
77, Lionel Messi ndio alikuwa hatari na kufanikiwa kufunga magoli mawili dakika
ya 33 na 90 baada ya Ivan Rakitic kufunga goli la pili dakika ya 73.
No comments:
Post a Comment