MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA VIONGOZI WA UWT ZANZIBAR

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa UWT kutoka mikoa minne ya Unguja.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa UWT Unguja ambapo aliwaambia washikamane katika kukitetea Chama kilichobeba maana halisi ya Mapinduzi na alihimiza Vijana wapewe nafasi kwa wingi kwani wao wananguvu na kasi ya siasa ya wakati huu.
 Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake,na Watoto Mhe, Maudline Castico akizungumza wakati wa mkutano wa Mjumbe wa Kamati Kuu CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Viongozi wa UWT Unguja .
 Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akizungumza kwenye mkutano wa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Viongozi wa UWT kwenye ukumbi wa NEC Afisi Kuu Kisiwandui, Zanzibar.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wasanii wa Filamu nchini maarufu kama Bongo Movie waliopita kumsabahi kwenye Makao Makuu ya CCM, Kisiwandui Zanzibar.

Source: habari za jamii

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search