RONALDO AIPELEKA KILIO BAYERN,.. MADRID WATINGA NUSU FAINALI UEFA; LEICESTER CITY YATUPWA NJE 


Mshambuliaji wa Real Madrid na Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo amefikisha mabao 103 aliyofunga katika michuano ya Ulaya ngazi ya klabu huku  akiingia uwanjani akiwa na mabao 100 baada ya kufunga mawili mjini Munich.
Bayern walianza kufunga bao la kwanza dakika ya 53 kwa mkwaju wa penalti kupitia Robetro Lewandowski, Madrid wakasawazisha dakika ya 76 akifunga Ronaldo kabla ya beki Sergio Ramos kujifunga dakika mbili baadaye.
Kipigo cha 2-1 kwa Madrid kilisababisha kuongezwa kwa dakika 30 na ndipo Madrid ilipoanza kuporomosha mvua ya mabao, Ronaldo akifunga dakika ya 106 kwa pasi ya Ramos na Marcelo akawachambua mabeki wanne kabla ya kumpa pasi safi Ronaldo aliyefunga bao la nne dakika ya 110.
Marco Asensio ndiye aliyefunga bao la nne katika dakika ya 112 na kumaliza kazi dhidi ya Bayern ambao walicheza pungufu kuanzia dakika ya 84 baada ya Arturo Vidal kupigwa “umeme”.
Real Madrid starting XI: Navas; Carvajal, Ramos, Nacho, Marcelo; Casemiro, Kroos, Modric; Isco, Benzema, Ronaldo
Substitutes: Kiko Casilla, James, Kovacic, Lucas Vazquez, Asensio, Morata, Danilo
Bayern Munich starting XI: Neuer, Lahm, Boateng, Hummels, Alaba, Robben, Alonso, Vidal, Thiago, Ribery, Lewandowski 
Substitutes: Ulreich, Bernat, Kimmich, Costa, Rafinha, Coman, Muller.
MATOKEO MENGINE
 
Leicester City imeaga michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Atletico Madrid.
Leicester ndiyo waliokuwa nyumbani na walilazimika kusawazisha kwa bao la Jammy Vardy ili kupata sare hiyo.
Kwa sare hiyo, maana yake Atletico Madrid imesonga mbele kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya ushindi wa 1-0 ikiwa nyumbani Vicente Cardelon jijini Madrid.
KIKOSI CHA Leicester City:
Schmeichel, Simpson, Morgan (Amartey), Benalouane (Chilwell), Fuchs, Mahrez, Ndidi, Drinkwater, Albrighton, Okazaki (Ulloa), Vardy
KIKOSI CHA Atletico Madrid:
 Oblak, Juanfran (Hernandez), Savic, Godin, Filipe Luis (Correa), Saul, Gabi, Gimenez, Koke, Carrasco (Torres), Griezmann

Source: fullshangwe blog

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search