VIDEO: WAZIRI MWAKYEMBE ALIVYOKUTANA NA BMT, BODI YA LIGI NA TFF MJINI DODOMA.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na ujumbe kutoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bodi ya Ligi kuu Tanzania Bara na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Mjini Dodoma leo Aprili 20, 2017. (wapili kulia ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhe. Anastazia Wambura.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (Kushoto) akizungumza na ujumbe kutoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bodi ya Ligi kuu Tanzania Bara na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Mjini Dodoma kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na ujumbe kutoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bodi ya Ligi kuu Tanzania Bara na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Mjini Dodoma kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe.
Mwanasheria wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Emmanuel Muga Agustino, (wapili kushoto), akifafanuamasuala ya kwa kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe(hayupo pichani) wakati wa kikao kati ya Waziri na ujumbe kutoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bodi ya Ligi kuu Tanzania Bara na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Mjini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura(kushoto) akieleza masuala mbalimbali yahusuyo Ligi Kuu Tanzania Bara kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe(hayupo pichani) wakati wa kikao kati ya Waziri na ujumbe kutoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bodi ya Ligi kuu Tanzania Bara na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Mjini Dodoma.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search