Dunia yasherehekea Mei Mosi kwa 'mabango' nimekuwekea picha kadha wa kadhaa za matukio ya fujo na maandamano yaliyotawala Mei Day katika nchi mbali mbali!


Wakati Watanzania tukisherehekea Siku ya Wafanyakazi Duniani kwa amani na  utulivu uliosheheni hotuba za matumaini kutoka kwa viongozi wetu wakiongozwa na Rais Magufuli, hali ililikuwa tofauti kwengineko wakati wakati vyama vya Wafanyakazi vikiungana  kufanya kufanya maandamano kupinga unyanyasaji na hali mbaya za kipato.



Nchini Uturuki zaidi ya watu 70 walikamatwa na askari wa kutuliza ghasia walipojaribu kuandamana nje ya jengo maarufu la Taskin Square lililopo katikati ya Jiji la Istambul wakidai ongezeko la mishahara na mazingira duni kwa Wafanyakazi.


Hali kama hiyo ilijitokeza pia Nchini Korea Kusini wakati maelfu ya Wafanyakazi waliovalia vikaragosi walitapakaa mitaani wakipiga kelele kuungana vyama vya Wafanyakazi kuishinikiza Serikali kupiga marufuku makampuni makubwa kukomesha ajira za muda (vibarua) kwa Wafanyakazi.
Fuatana na blogu yako ya Matukio ujionee hali ilivyokua katika miji mbali mbali duniani..










About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search