GOOD NEWS!! Tozo za Barabarani zimeshuka kwa asilimia 30.9 kwa wiki..

Jeshi La Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limekusanya kiasi cha Tsh. milioni 304 kutokana na tozo za makosa mbalimbali, ikiwa ni pungufu kwa 30.9% kutoka 440million zilizokusanywa kwa wiki iliyoishia Mei 21, 2017.

Kamanda Sirro
Hayo yameelezwa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Simon Sirro kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari mchana huu.

Mapungufu haya ya mapato kwa upande mmoja 'habari njema' na faraja miongoni mwa watumiaji wa barabara kwa tafsiri ya madereva kuwa waangalifu zaidi na kufuata kanuni zinazohimizwa na Jeshi la Polisi Nchini za 'Utii wa Sheria Bila Shuruti' hivyo kuepuka kukamatwa kwa makosa mbali mbali na kutozwa faini !!

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search