habari Njema: Ngozi ya Nguruwe yapata 'Mbadala' sasa Madaktari Watatumia Ngozi ya Samaki aina ya Sato kutibu Majeraha Makubwa ya Moto..kwa Binadamu !

Madaktari wa Nchini Brazil wamesema matumizi ya Ngozi ya Samaki aina ya Sato kutibu majeraha ya moto yameonyesha Mafanikio Makubwa. 

Wanasayansi hao wameongeza kuwa mbali kushabihiana sana na ngozi halisi, samaki hao pia wamebainika kuwa na kiwango kikubwa sana cha Madini ya 'collagen' na 'Protein' ambayo husaidia majeraha makubwa ya moto kupona haraka.



Wanasayansi hao wameanza rasmi kutumia njia hiyo inayodaiwa kuwa na ufanisi mkubwa zaidi ya kutumia bendeji za kawaida kwa kuwa ngozi ya Samaki hao inasaidia kupambana na maambukizi ya bakteria wanaoshambulia majeraha ya moto ikiwa na madini yanayosaidia kufuta alama za kuungua kwa haraka.

Inaelezwa mpaka sasa zaidi ya wagonjwa kadhaa waliotibiwa kwa kutumia ngozi ya Samaki hao wameonesha maendeleo mazuri. Kwa mujibu wa madaktari hao ufanisi huo utapunguza kwa kiwango kikubwa sana matumizi ya Ngozi ya Nguruwe ambayo sasa itatumika kwa matumizi madogo madogo ya kufungia vidonda n.k

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search