Kuna taarifa ya ajali mbaya ya basi aina ya Coaster likiwa limebeba wanafunzi maeneo ya Karatu
Tumepata taarifa muda huu kuna ajali mbaya imetokea maeneo ya karatu basi la shule limeanguka kabla ya kuingia karatu mjini na kuua watoto wengi ambao idadi yake bado haijafahamika. Wanafunzi hao wanaokadiriwa kuwa wa darasa la 7 inasemekana ni wa shule inayoitwa Lucky Vicent ya Arusha ambao walikua wanaenda karatu kufanya mitihani ya mashindano na shule za karatu. Kwa mujibu wa shuhuda basi hilo lilikua limebeba watoto zaidi ya 40 na wengi wao (zaidi ya nusu) inasemekana wamepoteza maisha akiwemo dereva na walimu… tuendelee kupashana kwa karibu na kuwaombea majeruhi
Source: JF
No comments:
Post a Comment