Mambo Makuu 8 yaliyopendekezwa na ‘Kamati ya Mchanga wa Madini’
Huu ni muhtasari wa kamati ya
uchunguzi wa mchanga wa madini kama ulivyowasilishwa na mwenyekiti wake Prof
Mruma hii leo Ikulu!.






Mawasilisho Ya Mwenyekiti wa Kamati, Prof. Mruma
1.Kamati ilikuwa na kazi ya
kuchunguza aina na kiwango cha madini yaliyopo ndani ya mchanga wa madini
unaosafirishwa nje!.
2.Chimbuko la utafiti huo ni
kutojulikana kwa kiwango cha makinikia na mikataba yake!.
3. Hadidu za rejea zilikuwa
,Kufanya uchunguzi wa makinikia kwenye bandari ya Dar es salaam na
migodini,Kufanya uchunguzi wa kimaabara ili kujua thamani na aina ya madini
yaliyopo kwenye makinikia,kuchunguza uwezo wa scanner zilizopo bandarini,kuchunguza
uwezo wa TMAA katika kusimamia makinikia,
4.Kamati ilitembelea bandari
ya Dar es salaam,bandari kavu na kwenye migodi ya Bulyanhuru na Buzwagi,yapo
makontena ambayo kamati ilichukua sampuli ya juu na chini,sampuli nyingine
ilikuwa zigzaga!.
5.Kamati ilichunguza uwezo wa
scanner kupima makinikia!.
6.Kamati ilikokotoa thamani ya
madini yaliyopatikana kwenye makinikia!.
MATOKEO YA UCHUNGUZI
1.Kamati imebaini uwepo wa
dhahabu kiasi Kikubwa cha dhahabu kwenye makinikia,katika makontena 277 yaliyozuiliwa
kulikuwa na tani saba za dhahabu!.
2.Makontena 277 yaliyozuliwa yalikuwa na dhahabu yenye thamani zaidi ya shilingi Trilioni moja nukta moja nne saba!.
2.Makontena 277 yaliyozuliwa yalikuwa na dhahabu yenye thamani zaidi ya shilingi Trilioni moja nukta moja nne saba!.
3.Kamati ilibaini uwepo wa
madini ya shaba,Silver,surpher,chuma.
4.Copper pekee ilikuwa ya thamani
ya shilingi Bilioni 23.3,hapa kulikuwa na tofauti kubwa na ripoti ya serikali
ambayo ilionesha kuwa na thamani ya Bilioni 13.
4.Upande wa silver kamati
ilibaini uwepo wa silver ya thamani ya bilioni 2.1.tofauti na ripoti ya
Serikali ilionesha thamani ya Bilioni 1.
5.Upande wa surpher kamati
ilibaini uwepo wa surpher ya thamani ya shilingi bilioni 1.9,kamati ilibaini
madini madini haya hayapo katika mrabaha
6.Kamati ilibaini uwepo wa
madini ya chuma yenye thamani ya shilingi Bilioni 2.3,
7.Kamati ilibaini uwepo wa
madini mkakati ambayo kwa sasa yanahitajika sana duniani yenye thamani kati ya
bilioni 129.5 mpaka bilioni 261.5
Thamani ya madini yote katika
makinikia kwenye makontena 277 yaliyochunguzwa kamati imebaini yana thamani ya
triloni 1.339,ambazo serikali haipati hasa senti moja na hayapo kwenye
mrabaha!.
8.Kamati imegundua uwepo wa
madini mengine mengii ambayo hayarekodiwi kwenye nyaraka za serikali!.
9.Kamati imebaini wakala wa
madini Tanzania hawafungi utepe kwenye makontena kuonesha viwango vya
madini,kamati imebaini ufungwaji huu kufanyika wakati wa kusafirisha makontena.
10.Kamati imebaini scanner za
bandarini kutokuwa na uwepo wa kubaini utotoshwaji wa mali!.
MAPENDEKEZO YA KAMATI
1.Serikali isitishe
usafirishaji wa mchanga nje ya nchi
2.Serikali ihakikishe mitambo
ya kusafisha makinikia unafanyika nchini
3.TMAA ifunge utepe mara baada
ya mchanga kupakiwa kwenye makontena!.
4.TMAA ipime metal zote kwenye
makininia
5.TMAA ipime viwango vyote vya
makinikia na madini kwenye maabara bila kujali ripoti ya msafirishaji hii
itasaidia Serikali kupata mrabaha!.
6.Serikali iwachukulie hatua
watendaji wa TMAA na wizara husika.
7.Serikali iweke mfumo
kushtukiza kwenye udhibiti wa madini!.
8.Serikali itumie wataalam wa
mionzi kwenye scanner za bandarini!.
Source: John Bukuku wa Fullshangwe blog.

Rais Dk John Pombe Magufuli akipokea ripoti kutoka kwa Profesa Abdulkarim Hamis Mruma Mwenyekiti wa Kamati Maalum ambayo ilipewa kazi ya kuchunguza kiwango cha aina ya madini yaliyomo kwenye mchanga uliomo ndani ya makontena yaliyozuiliwa na Serikali Bandarini na sehemu mbalimbali hapa nchini hafla hiyo imefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 24/5/2017, Katikati ni Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan na kulia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Mh. Kassim Majaliwa
!.

Rais Dk John Pombe Magufuli akielekezwa jambo wakati akipokea ripoti ya ukaguzi kutoka kwa Profesa Abdulkarim Hamis Mruma Mwenyekiti wa Kamati Maalum ambayo ilipewa kazi ya kuchunguza kiwango cha aina ya madini yaliyomo kwenye mchanga uliomo ndani ya makontena yaliyozuiliwa na Serikali Bandarini na sehemu mbalimbali hapa nchini Ikulu jijini Dar es Salaam, Katikati ni Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan na kulia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Mh. Kassim Majaliwa.

Rais Dk John Pombe Magufuli akizungumza wakati akipokea ripoti ya ukaguzi wa madini katika makontena hayo Katikati Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na kulia ni Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan.

Profesa Abdulkarim Hamis Mruma Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya kuchunguza Madini katika Mchanga ulioko kwenye makontena ambayo yamezuiliwa maeneo mbalimbali nchini akizungumza wakati wakiwasilisha ripoti hiyo Ikulu jijini Dar es salaam leo

Rais Dk John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan wakifuatilia kwa makini wakati Profesa Abdulkarim Hamis Mruma Mwenyekiti wa Kamati Maalum ambayo ilipewa kazi ya kuchunguza kiwango cha aina ya madini yaliyomo kwenye mchanga uliomo ndani ya makontena yaliyozuiliwa na Serikali Bandarini na sehemu mbalimbali hapa nchini alipokuwa akiwasilisha ripoti hiyo.

Rais Dk John Pombe Magufuli , Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa wakifuatilia kwa makini wakati Profesa Abdulkarim Hamis Mruma Mwenyekiti wa Kamati hayupo pichani alipokuwa akiwasilisha ripoti hiyo.

Rais Dk John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi mbalimbali wa serikali mara baada ya kupokea ripoti hiyo.

Waimbaji Frora Mbasha, Kalala Junior na Shilole pamoja na wenzao wakitumbuiza wimbo maalum wakati wa kuwasilishwa kwa ripoti hiyo.

Wasanii mbalimbali wakitumbuiza wakati wa uwasilishwaji wa Ripoti hiyo Ikulu leo jijini Dar es salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk John Pombe Magufuli akiwapongeza wanasanii hao mara baada ya kuimba wimbo maalum wa kuhamasisha uzalendo kwa nchi Iukulu leo.

Rais Dk John Pombe Magufuli akimpongeza MwanaFA na wenzake.

Rais Dk John Pombe Magufuli akimpongeza Frola Mbasha na wenzake mara baada ya kuimba wimbo maalum wa kuhamasisha watanzania kuwa wazalendo mara baada ya kupokea ripoti hiyo.

Baadhi ya viongozi mbalimbali wa srikali , Dini, vyombo vya Ulinzi na Usalama wakiwa katika hafla hiyo.

Wasanii mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu leo.


Rais Dk John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wasanii

Rais Dk John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa vyama vya Siasa.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akizungumza na Kiongozi wa Kanisa la KKKT Kanda ya Mashariki na Pwani Dk Alex Malasusa.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalaam Jenerari Venance Mabeyo akisalimiana na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Sheikh Al- Hadi Salum Musa

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akisalimiana na Mwanamuziki Peter Msechu.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akisalimiana na wadau Muhidin Michuzi katikati na Adam Gille wakati walipokutana Ikulu leo katika hafla ya uwasilishwaji wa Ripoti ya uchunguzi wa Kamontena ya Mchanga yaliyozuiliwa Bandarini na maeneo mbalimbali nchini.

Picha mbalimbali zikionyesha Rais Dk John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kupokea ripoti ya uchunguzi wa Kamontena ya Mchanga yaliyozuiliwa Bandarini na maeneo mbalimbali nchini.






No comments:
Post a Comment