'Kubeti' kunavyowatafuna 'MASTAA' Wayne Rooney aliwa Billion 2 ndani ya masaa mawili!


Ndugu msomaji wa matukio blog,.. hebu vuta picha umedondosha 'wallet' yako yenye kiasi cha Sh. 100,000/ usawa huu.. bila shaka utajisikia 'usongo' sana. Sasa hali ni tofauti kabisa kwa 'Staa Wayne Rooney' ambae usiku wa kuamkia jana alitinga ndani ya klabu 235 Casino mjini Manchester na kuteketeza kiasi cha pauni 500,000 za Uingereza ambazo ni chini kidogo ya Billion 2 kwa pesa za kibongo.



Mpashaji habari wa gazeti maarufu la The Sun ambalo lilishuhudia Rooney alitinga Casinoni humo akiwa chakari mida saa 6 usiku akiruka mashine hii na ile bila kuwa na mpangilio maalum huku wahudumu wakijitahidi 'kujishebedua' kumpa hadhi yake ya VIP Casinoni hapo bila yeye kuonekana kujadi.
Rooney aliendelea kudanda counter hadi counter, mashine  hadi mashine, 'slot' hadi 'slot' akiitafuta fortune,.. huku akiendelea kuliwa mamia kwa maelfu ya pesa kila dakika na sekunde iliyokwenda kwa Mungu... na mpaka akitoka maeneo hayo mida ya saa 8 usiku tayari alishaliwa kiasi hicho cha £500,000 ambazo ni nyingi sana kwa pesa za Bongo au 'madafu'
Wakati wote huo mke wa Rooney aitwae Coleen na watoto wao Kai, Klay na Kit walionekana wakijivinjari maeneo mengine kabisa wakati 'baba wa familia' akiambulia maumivu hayo..
Wakala wa mchezaji huyo nyota wa Mashetani Wekundu wa Nchini Uingereza hakushtushwa na hasara aliyoipata Rooney kwani ni hobby ya mastaa wengi wa mpira na kuthibitisha kuwa kuna kipindi Rooney aliliwa £650,000 Casinoni hapo ambazo ni pesa za kibongo SHS.2.8billion ndani usiku mmoja.
Nae mhudumu mmoja alieficha utambilisho wake alisema hii ni klabu ya mastaa na akawataja Rio Ferdinand, Ryan Giggs, na wacheza sinema Kym Marsh na Michelle Keegan miongoni mwa mastaa wasiobanduka Casino 235.

Ndugu msomaji nakupa hii homework hapa: tazama picha za Rooney akiwa Casino235 jana kisha jaza maoni yako kupitia:www.tanzaniampyamatukio.blogspot.com

Ciaoooo!!!





endelea kufuatilia blog yako ya matukio: 
www.tanzaniampyamatukio.blogspot.com

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search