Kuelewana ni kuzungumza: Kim akubali yaishe, sasa asema yuko tayari kwa maongezi na Donald Trump.

Rais Wa Korea Kaskazini Kim Jong un
Korea Kaskazini imesema kuwa itafanya mazungumzo na Marekani iwapo mazigira yataruhusu ,kulingana na vyombo vya habari vya Korea Kusini.
Mjumbe mwandamizi wa Korea Kaskazini amesema kuwa mazungumzo na serikali ya rais Trump yanawezekana kufuatia mkutano na waliokuwa maafisa wa serikali ya Marekani nchini Norway.
Awali mwezi huu rais wa Marekani Donald Trump alisema itakuwa heshima kubwa kukutana na rais Kim Jong un.
Matamshi yake yanajiri kufuatia ongezeko la hali ya wasiwasi kuhusu mipango ya Korea Kaskazini ya kinyuklia pamoja na ile ya utengezaji wa makombora ya masafa marefu.
Choe Son Hui ambaye ni afisa katika wizara ya maswala ya kigeni kuhusu maswala ya Marekani kaskazini alitoa matamshi hayo wakati alipokuwa akirudi Pyongyang baada ya mkutano mjini Oslo.- bbc swahili

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search