SAD NEWS!!! Mkuu wa Polisi Uvinza auawa kikatili Jijini Dar es Salaam..
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Uvinza, Amedius Malenge ameuawa nyumbani kwake Kinyerezi Kanga wilayanin Ilala. Akizungumza jioni hii Shemeji wa Marehemu, Reginald Lyimo alisema Marehemu alikuja Dar es Salaam kwa ajili ya sherehe ya kumuaga Binti yake iliyofanyika Alhamisi iliyopita.
Akiongelea mkasa huo alieleza Malenge alihamishiwa wilaya ya Uvinza akitokea wilaya Kibaha alikokuwa afisa upelelezi wa wilaya.Alisema alimalizia nyumba yake hivi karibuni ili familia yake ibaki Dar es Salaam na walikuwa bado hawajahamia,.. tulkuwa nae Alhamis tukisherehekea kuolewa kwa binti yake Prisca lakini anakuja kuuawa kikatili namna hii," alimalizia kuongea kwa masikitiko... Alisema baada ya kuagana kwenye harusi hiyo walipanga juzi kwenda Kibaha kwa ajili ya kuwashukuru wafanyakazi wenzake waliomchangia katika harusi hiyo.
Tutaendelea kuwajuza kupitia blog yako ya matukio: www.tanzaniampyamatukio.blogspot.com
No comments:
Post a Comment