Video: 'Mwanzo Mwisho' wa Kisa cha Mtoto anaekunywa Mafuta kama 'mlo wake mkuu'
Kwa hisani ya 'Mtu wa Nguvu' tumekuwekea kisa kuhusu mtoto Shukuru Kisongamwenye umri wa miaka 16 mkaazi wa Tunduru ambaye ameishi kwa kunywa mafuta ya kula lita moja, maziwa lita mbili na sukari robo tatu kwa siku.
Siku chache zilizopita Shukuru ambaye ni mwanafunzi wa Kidato cha Pili alifikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es salaam kwa ajili ya matibabu kutokana na tatizo hilo.
Leo May 23, 2017 Dokta Stella Rwezaura ambaye anamtibu mtoto Shukuru, amekutana na waandishi wa habari kwa ajili ya kuelezea juu ya ugonjwa wa unaomsumbua mtoto huyo akisema baada ya kumfanyia uchunguzi wamebaini anasumbuliwa na Selimundu ‘sickle cell’.
Aidha, Dkt. Rwezaura ameongeza kuwa kwa sasa mtoto Shukuru ameacha kutumia mafuta ya kula na Sukari na kuanza kutumia uji…yapo mengi aliyoyaeleza Dkt. Rwezaura kwenye video hii hapa chini ambayo unaweza kuitazama kwa ku-play….
No comments:
Post a Comment