Video: Mapya yaibuka sakata la “Grenfell Tower inferno” #share.. Mkaguzi, Wapangaji waelezea msururu wa ishara kuelekea moto wa maangamizi..



Wakazi manusura wa mkasa wa moto wa jengo la Grenfell jijini London, wameelezea mtiririko wa matukio ya hivi karibuni yaliyotoa ishara ya mkasa mbaya katika jengo lao katika siku za karibuni, kabla ya ishara hizo kugeuka na kuwa mkasa wa maangamizi mazito ulioandika historia ya moto katika jiji hilo baada ya ule wa ‘london fire’ au ‘Wood Fire’ kama ulivyotambulika sana.


Hadi sasa imethibitishwa na Polisi  nchini humo, jumla ya watu 12 wameshafariki huku juhudi za kutafuta maiti zaidi zikiendelea, ambapo watu 79 wamelazwa hospitalini kwa matibabu Zaidi huku 18 wakiwa mahututi. 

Wakisimulia mkasa mzima, baadhi ya wapangaji pamekuwa na maonyo mbali mbali kutoka kwa watu wasiofahamika, likiwemo onyo la hivi karibuni kabisa ambapo vikaratasi vingi vilitawanywa katika jengo hilo vikiwaonya wasitoke nje ya vyumba vyao endapo tukio lolote la moto litatokea ili kuwapa nafasi wafanyakazi wa uokoji kufanya shughuli za uokoaji kwa njia rahisi Zaidi.

Wakazi hao wameonya jengo lao lenye wakazi 600 halikuwa na vifaa vyovyote vya kuzima wala ving’ora vya kutoa ishara pindipo moto utatokea.
Kumekuwepo na hisia kadhaa pia za mawaziri husika wa mambo ya makaazi, majengo na usalama wa ndani kudharau vilio vya wananchi wengi wanaolalamikia wenye majengo juu ya ukosefu wa usalama wa kutosha.

Mkaguzi Mwandamizi wa Majengo Jijini London Eng. Sam Web ambae alilikagua jengo la Grenfell baada ya ukarabati mkubwa wa hivi karibuni uliogharimu kiasi cha Pauni Million 10, alilipa jengo hilo alama 40 tu chini ya 100 juu ya usalama na udhibiti wa moto na kukosoa mapambo mengi ya plastiki (Plastic Cladding) yaliyozungushiwa Grenfell kuwa ni ‘kuni zilizosubiri kuwaka..


Grenfell Tower baada ya ukarabati wa Pauni 10 million

Grenfell ya zamani iliyojengwa mwaka 1974

Grenfell ya leo baada ya kuteketea kwa moto wa jana !

Askari wa zima moto wakiendelea na kazi ya kutafuta miili

wasaidizi wa kutoa huduma wakiendelea kuto miili baada ya kunasa ndani ya jengo la Grenfell

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search