Baada ya Mbunge Nkamia 'kutibua hali ya hewa' kwa hoja ya u-Rais kuwa Miaka 7... Mbunge Henche Chadema kamjibu na hoja ya ukomo wa u-Rais wa miaka 4... Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360...#share
SIKU chache baada ya Mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kutangaza dhamira yake ya kuwasilisha hoja binafsi Bungeni ya kutaka kuongezwa kwa muda wa Rais kuwa madarakati kutoa miaka mitano ya hivi sasa hadi saba.
Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche naye ameonyesha dhamira yake ya kupeleka hoja binafsi bungeni ya kupunguza muda wa kuwa madarakani kwa Wabunge na Madiwani kutoka miaka mitano hadi ya hivi sasa hadi minne.
"Nakusudia kuwasilisha bungeni hoja binafsi kupunguza mda wa kukaa madarakani kwa rais, wabunge na madiwani kutoka miaka 5 mpaka 4 tuwe kama Marekani ili kutoa nafasi kwa wananchi kuwa na maamuzi zaidi kuhusu uendeshaji wa nchi yao," ameandika Heche kupitia ukurasa wake wa faceebook.
Hivi karibuni Nkamia alithibitisha dhamira yake ya kutaka kupeleka hoja binafsi ya kuhusu ukomo wa muda wa Rais Kuwa Madarakani uongezwe kutoka miaka mitano ya hivi sasa hadi miaka 7 kama ilivyo kwa nchi ya Rwanda, jambo ambalo lilizua mjadala mkubwa nchini huku walowengi wakipinga hoja hiyo kwani inataka kusababisha uvunjifu mkubwa wakatiba.
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment