Exclusive:(+Audio) Maajabu ya Msukule - Msanii Popo Michael wa Geita afariki na kuzikwa, kisha apatikana Nyankumbu akiwa hai.. haya hapa ndio mahojiano yake na mwandishi maalum wa Matukio360.. #share
MSANII wa nyimbo za asili mkoani Geita Daniel Matunge almaarufu kama Popo Michael anaishi katika hali ya mateso kutokana na
kile alichoeleza kusafirishwa kwa njia ya aanga kimazingara kutoka Kahama
Mkoani Shinyanga hadi Nyankumbu mkoani Geita huku wazazi wake wakiwa na
taarifa za kuwa amefariki dunia.
Akizungumza kwa taabu nyumbani kwa baba yake mdogo Paschal
Matunge katka kijiji cha Mwenegeza kata ya Nyakagomba tarafa ya Butundwe ,
Msanii huyo alijikuta katika hali isiyoeeweka akiwa mjini Kahama Mkoani
Shinyanga baada ya kusalimiana na watu wawili mke na mme ambao hakuwatambua.
Ameelza kuanzia hapo alijikuta akiwa angani katika chombo kisichofahamika na kutupwa
chini katika ardhi ya Nyankumbu mkoani Geita.
Amesema tukio hilo lilimkuta siku ya Ijumaa, na akaokotwa siku
ya jumamosi majira ya asubuhi akiwa na pamba mdomoni, puani na masikioni mithili
ya maiti.
Baba mzazi wa Msanii huyo Michael Matunge
amesema kabla ya kuokotwa kwa mtoto wake, alipokea simu na ujumbe wa maadishi
sms ukimtaarifu kuwa kijana wake amefariki na kwamba mwili wa marehemu upo
katika Hospitali ya wilaya Kahama ambapo ndugu zake walifuatilia nakubaini kuwa ni uwongo.
Msanii huyo anayefahamika kwa jina la Popo Michael ana wake
wawili.
Hamisa Sadiq ni mke mkubwa, anahusisha tukio hilo na imani za kishirikina kwa kuwa siku ya
Ijumaa usiku alimuona mme wake akiwa ndani amekaa kwenye kiti, na alipotoka nje
kwaajili ya haja ndogo hakumuta hadi asubuhi zilipopatikana taarifa kuwa
amefariki na mwili kuokotwa Nyankubu ukiwa na pamba masikioni, puani na mdomoni.
Hata hivyo, Daniel Michael Matunge almaarufu kama Popo
Michael anaeleza kuwa kutokana na kudondoshwa chini akitoka angani kwenye
chombo cha usafiri ambao hakukitaja anaumia sehemu mbali mbali za mwili kama
vile,Mgongo,kiuno,miguu,kichwa na shingo.
No comments:
Post a Comment