Profesa Jay Atia Neno Saka la Zari, Diamond na Hamisa Mabetto...Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360...#share
MBUNGE wa
Mikumi mkoani Morogoro na Mwanamuziki nguli wa wa HipHop nchini Joseph Haule a.k.a Professor Jay amemuunga
mkono msanii wa muziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwa
kitendo chake cha kuweka wazi kuwa mtoto wa Mwanamitindo Hamisa Mobetto ni wake.
Profesa Kupitia
mitandao yake ya kijamii ya Instagram na Facebook ameandika maneno haya “Ukweli humuweka Mtu huru KWELIKWELI.. Big up
mdogo wangu @diamondplatnumz Umekuwa Mfano bora sana.”
Itakumbukwa jana
Diamond akiweka wazi suala hilo wakati akiendelea
na mahojiano katika kituo cha Clouds FM, Zari aliandika katika mtandao huo
akisema, “Hahahaha unajidanganya, unasema
uongo kuhusu mimi kujua kuhusu michepuko yako, malizana na balaa
ulilolianzisha. Mimi kunyamaza haimaanishi ni mpumbavu. Kuwa makini na maneno
yako.”
Aliendelea kuandika: “Inawezekana
mimi ni mama wa watoto wako ndio maana nimeamua kunyamaza kimya. Labda ugoogle
kuhusu ‘defamation of character law suit’, usinijaribu.”
Na Mwandishi wetu
No comments:
Post a Comment